Natumia fursa hii kuwazindua vijana kuamka kutoka katika lepe la usingizi wa mawazo, nimeamua kuzungumza na vijana kwakua bado wananafasi kubwa sana katika utafutaji wa maisha, inamaana, wana kila kitu muhimu katika nyenzo za kutafuta, inamaanishwa, nguvu,akili imara,maarifa nk, lakusikitisha wengi wao ni kama vile wamelala fofofo.
Ifahamike katika maisha, kuna muda wa kujifunza, kuna muda wa
kutafuta na kuna muda wa kutumia.
Sasa hapa wengi ndio hufeli kwa kuchanganya
nyakati hizi,ili ufanikiwe ni lazima upitie nyakati hizi kwa utaratubu wa kama
ilivyoainishwa katika ujumbe juu, kwanza ujifunze, nakusudia elimu,baadae
uchakarike kisha ndio ule matunda ya ulichokipanda, Sitaki kueleza sana katika
hili mana siko nilipokusudia, lakini huu uchache wake utakusaidia sana, ukiamua
kubadilika.
Jitahidi unaposoma post hii, ikili yako, ufungamanaishe na hamu ya
kutaka kufanikiwa, na azimia katika nafsi yako, unasoma kisha unatekeleza kwa
vitendo uliyoyasoma,itakusaidia. Lilikokusudiwa ni kama ilivyoelezwa hapo awali
katika aya ya kwanza ni kuwa, vijana ni wakati wenu sasa kuamka, na leo
niyayaeleza makosa machache kati ya mengi yanayofanywa ambayo hurudisha nyuma
malengo ya viajana na vipi vya kufanya ili kufanikiwa katika maisha,usiache
kusoma mpaka mwisho na hii ni posto yenye mtindo wa mwendelezo kila baada ya
siku mbili.
Ni kwamba, hatukuja duniani kutembea, kwa wafuasi wa dini ya
kiisilamu ni kua tupo kwaajili ya kufanya Ibada na moja miongoni mwa ibada ni
kufanya kazi, na si uisilamu pekee, dini yoyote duniani inahimiza kufanya kazi
na mafanikio. Na katika muktadha wa ufanyaji kazi inazingatiwa kitu "TIJA" yaani
mafanikio ambayo kwa harakaraka tunasema ni kufikia lengo la kazi unayoifanya,
ikiwa ni kupata pesa, hadhi, au chenginecho.
Kimsingi vijana wengi wa siku hizi
wanalalamika maisha ni magumu na baadhi yao husema hawafanyi kazi kwakua hawana
kazi, nihivi , ukibaki kuwa na mawazo haya kila siku,utaendelea kubakia
hivyohivyo kila siku, utazikwa na watu watakusahau,kazi zipo, acha kufikiria
ndani ya boksi, toka na fikiria nje ya boksi.(katika matoleo mengine utafahamu
namna ya kufikiria nje ya boksi na mafakio yake) Unajua ni kwanini vijana wengi
wanasema hakuna kazi, ni kwasababu hizi zifuatazo.
Kwanza, wapo
waliyojiaminisha, wao ni watu wa kazi fulani tu na kazi fulani haziwahusu, zina
watu maalum, kama vile kilimo, wapo wanajiona wao hawastahiki kabisa kuwemo
katika fani hii (Kilimo ndio mada kuu katika posti hii, itafafanuliwa vizuri
baadae).
Pili, wapo wanaoangalia jamii zinazowazunguka eti wataasemwa
vibaya,wanaona aibu kufanya kazi fulani kwakua ametokea katika familia yenye
hadhi fulani , huu ni ujinga na kama unatabia hii huwezi kufanikiwa, acha
kabisa, geuza fikra zako, maisha ni yako wewe sio yao, kila mmoja ana yake,
alimradi utakachokifanya hakiendi kinyume na serikali na dini yako.
Wengine ni
watu wa kughairisha kila jambo, hawana kitulizano katika mambo yao, na wanakua
na papara katika kuyataka mafanikio.Kijana kumbuka, mafanikio ni mchakato na sio
tendo, hakuna njia ya mkato katika mafanikio, kaa, tulia, waza, umia, kua na
uhimulivu (sustainability) katika kazi yako.
Mfuatialiaji wa ZenjiUpdate, hii ni
post ya awali katika andiko hili, naamini kama utaendelea kufuatilia toleo
jengine na mpaka utakapomaliza utajifunza mengi, na hatimae utabadilika na
kuamka kutoka usingizini, usiache kufuatilia, lengo ni kufanikiwa, njia zipo za
rahisi za kuzipita kikubwa ni uvumilivu. Waliyofanikiwa ni binaadamu kama
wewe,hawana kiungo kipya cha ziada katika miili yao, nawe unaweza kuwafikia,
usife moyo.
0 Comments