Imeandikwa na Nusra Shaaban - Zanzibar
Katika kuwasaidia Vijana na kujitambua,Mkuu wa mawasiliano kutoka chuo cha uandishi wa habari Kilichopo kilimani Zanzibar Imane Os Duwe ambae pia ni Mwalimu na Mshauri wa vijana ametoa mafunzo ya kujitambua kwa vijana ili kuwasaidia kuishi kwa malengo na kufikia ndoto zao...
Katika mafunzo aliyoyatoa huko katika ukumbi wa Rahaleo studio siku ya Jumamosi ya tarehe 2Julai mwaka huu Mwalimu Imane amesema vijana wanakila sababu ya kufanikisha malengo yao endapo tu watajitambua wao ni nani na nini wanakihitaji maishani mwao...
Ameongeza kwa kuwashauri vijana kuendelea kujiamini ili kujenga uwezo wa kuamua mambo yaliyo sahihi maishani mwao...
Baadhi ya vijana waliopatiwa mafunzo hayo wamesema wamepata taaluma ya kuendelea kujiamini na kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuzichukulia kama ni fursa kwao.
0 Comments