Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu aitaka jamii kutowaita majina yasiyosahihi wenye ulemavu.

 Na Tatu Juma Zanzibar

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake  wenye ulemavu Zanzibar Bi Salma Ali Saadat aitaka jamii kutowaita majina yasiyosahihi watu wenye ulemavu.

Hayo ameyasema wakati akitoa 
mafunzo  kwa waandishi wa habar kuhusu habari za ujumuishi na haki za watu wenye ulemavu huko Ofisi ya Chama cha waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar  Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema kuwa kuna baadhi ya majina yanatumika katika jamii kuwaita watu wenye ulemavu ambayo hayastahili hivyo nivyema waandishi wakawa njia sahihi ya kupiga vita majina kama hayo."kuna majina kama vile viwete,vipofu, kiguru, dishi limeyumba,chongo namengi mengineyo" haya sio sahihi nivyema kutafuta mbinu mbadala ya kuondoa tabia hiyo katika jamii" amesema Bi Salma 

Hata hivyo amesema nivyema waandishi wa habari  wakafahamu zaidi haki za watu wenye ulemavu ili iwe njia moja wapo yakuielewesha jamii kuwa watu wenye ulemavu  wanathaminika na kupata haki sawa kama wengine.

Nae Afisa Mawasiliano kutoka TAMWA Zanzibar Khairat Ali amesema  lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu waandishi kuhusu maswala ya ujumuishi pamoja na haki za watu wenye ulemavu ili kuzifanyia utetezi  katika jamii.

Akitoa maoni kwa waandishi hao amesema ulemavu nihali yakibinaadamu hivyo haimzuii mtu kutopata haki zamsingi hivyo nivyema waandishi hao kuyapokea vyema mafunzo hayo nakuielewesha  jamii iweze kuelewa haki za watu wenye ulemavu kwa ufasaha.

Mafunzo hayo yasiku tatu  yaliyojumuisha waandishi thelethini
ambayo yanatekelezwa chini ya Program Action for Disability Right  kwakushirikiana na TAMWA Zanzibar na Norway.

Post a Comment

0 Comments