Ulinzi kwa Waandishi wa Habari ni Jambo la kwanza kabla ya mengine.

 Imeandikwa na Maryam Nassor  - Zanzibar 


WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kujihakikishia ulinzi na Usalama wao kwanza  kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu wa  Oktoba  mwaka huu.

Wito huo, umetolewa  August 6, 2025  huko katika Afisi za TAMWA ZNZ Tunguu , na mkufunzi wa Mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa Habari wa Unguja Maryam  Nassor akimuwakilisha ToT Najjat Omar kutoka klabu ya wandishi wa Habari Zanzibar ( ZPC).  

 Amesema , ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari  unaanza na  yeye mwenyewe hivyo ni lazima kujihakikishia ulinzi  na usalama  , huku wakizingatia  kunaelekea katika  kipindi cha uchaguzi mkuu ambacho ni hatarishi kwa wandishi wa Habari.

“ Waandishi lazima muwe makini katika kipindi hichi tunachoelekea kwani musipokuwa makini munaweza kuingia  kwenye matatizo  na kuhatarisha  maisha yenu “ amesema mkufunzi huyo.

Aidha amewataka wandishi wa  Habari kujilinda pia katika mitandao ya kijamii na kujiepusha kufungua viunganishi ( links) ambavyo sio  salama na hawajui vinapotoka.

 Amesema kuwa,   ni vyema wandishi wa Habari kulinda taarifa zao binafsi  zisifike kwa watu wasiohusika ili kuzuwia  udukuzi  na wizi wa taarifa.

 Nao baadhi ya wandishi waliyobahatika kupata mafunzo  hayo, Jesse Mikofu kutoka gazeti la mwananchi Zanzibar ameshauri ni vyema elimu kama hiyo kupewa na wamiliki wa vyombo vya Habari ili kusaidia kuwapatia vitendea kazi ambavyo vitasaidia kuwalinda.

 

Amesema kuwa, vyombo vingi vya Habari hawahamasishi waandishi wao, kuwa na vifaa vya kujilinda kama Press Jacket   na vyenginevyo wakati wa majanga.

 

Nae,  mshiriki  Samira Abdalla  kutoka  online ya ZU, ameshukuru kupatiwa mafunzo hayo  ya ulinzi na usalama  hasa kuelekea kipindi hichi cha uchaguzi, na kuahidi kuyafanyia kazi.

 

Mafunzo hayo ya siku mbili  kwa waandishi wa  Habari yanalenga  kumasisha  ulinzi na usalama kwa wandishi wa Habari kuelekea kipindi cha uchaguzi.

                             mwisho    

Post a Comment

0 Comments