WANAVYUO HALAHALA NA MAKSI ZA KUGAIWA NA HATARI YA KUDHALILISHWA

NA KHAULAT SULEIMAN-PEMBA
Baadhi ya wanafunzi wa kike vyuoni hawajitumi, ila wanatumia visa kama vile kukubali kuwa mpenzi wa wanahadhiri kwa minajisi ya kusaidiwa kitaalamu.
Hii ni kutokana na kukosa uamini wakati wa kusoma na kutofanyajitihada, katika masomo na kupelekea kutegemea misaada, ya kupata kiwango cha juu ya ufaulu.
Kukosa uwelewa na kujisahaulisha malengo husika yaliyokusudiwa kwa mwanafunzi wa chuo na kupelekea kujenga tamaa ya kingono ili kupasi katika mitihani yao.

JITIHADA ZA VYUONI.

Kama sehemu moja wapo ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia,tasisi nying za elimu ya juu zimechukuwa hatua za kuzuiya ukukwaji wa madili ikiwemo kuanzisha kanuni na madili ya wafanyakazi kutunga sheria ndogo ndogo za wananchuo na kua na sera ya jinsia.
"Ni pale tu ambapo mtoa rushwa asiporidhika ndipo anaweza kutoa tarifa kwa vyombo husika.
Kutokana na hali hiyo ya usiri muandishi wa makala hii alifanya uchunguzi katika baadhi ya vyuo vya mkoa wa kaskazini Pemba ili kubaini matendo ya udhalilishaji wa kijinsia katika sehemu za vyuo.
Ali Mussa mwalimu wa chuo cha WIARC Pemba, anasema hali ya udhalilishaji vyuoni kwa upande wa Pemba, jambo geni miongoni mwao.
Anasema, bado wanafunzi na waalimu, wamekuwa na  madili na misingi ya dini husasa walio wengi ni waislamu, wamekuwa wakichunga heshima zao.
"Naweza kusema labda wao wenyewe wanafunzi wadhalilishane kwa kudanganyana wakati hawana malengo yoyote, hii ni kutokana na kuendekeza ujana wao,’’anasema.
Amina Juma mwanafunzi wa chuo cha Afya Wete, anasema  kutokana na masomo kua magumu, ilibidi tu wapambane na masomo na kuachana na mapenzi.
"Lakini wapo ambao wao wanajifanya watoto wa mjini wanatafuta wanaume, nje na hata hapa chuoni na ndipo wanapofeli, maana huwa hawana malengo,’’anasema.
Shadya Mohamed aliyekua mwanafunzi katika chuo cha Kiislamu kiuyu ‘CCK’ alisema kuwa udhalilishaji katika vyuo mara nyingi, unategemea na mwanafunzi mwenyew sio kama waalimu .
Anasema, wapo wanafunzi ambao malengo yao ni mafupi, na wakati mwingine hudoea maksi za bure kwa waalimu wasio na maadili na kusababusha udhalilishaji.
Mwanafunzi Haitham Juma Hamad wa Chuo Kikuu Huria Tanzania tawi la Pemba, anakiri kuwa mwenzake mmoja, kwa sasa ameacha chuo baada, ya kutaka apewa alama za bure mwalimu, ambae alikuwa na maadili.
‘’Mwalimu alimtaka mwanafunzi asome kwa bidii, na hakuna alama za bure, hilo yeye lilimuumiza na kuacha masomo mwaka wa pili,’’anafafanua.

SERIKALI

Suala la rushwa ya ngono na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa vyuo wa vya elimu ya juu lilishawahi kuibuka bungeni mwaka 2006, kufuatia suala lililouzwa na mbunge wa jimbo la Kwamtipura Zuber Ali Maulid wakati huo.
Akijibu kwa niaba ya Waziri, aliyekua Naibu waziri wa Sayansi Tecknolojia na elimu ya juu Guadensia Kabaka alisema, ni kweli kuna uvumi kuwa katika baadhi ya vyuo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.
Hata hivyo, alisema kwa baadhi ya vyuo kuomba msaada wa uchunguzi, kutoka taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (Takukuru), bado kumekuwepo ugumu kuwabaini kutokana na kuwepo kwa usiri mkubwa.
Afisa mdhamini wizara ya elimu Pemba Mohammed Nassor Salim aliendelea kuwasisitiza wanafunzi kila wanapo fika katika skuli zao kutoa tarifa yoyote ambayo inashiria maswa ya udhalilishaji kwa endapo watafanya hivyo itawasabishia kutofikia malengo yao.

TAKWIMU 

Takwimu za udhalishaji mkoa wa kaskazini vinaonesha makosa 29 yanaendelea na upelelelezi ya ubakaji na kulawiti matatu na katika hayo hamna ata moja yaliyoripotiwa kutoka vyuoni.
Zanzibar ina zaidi ya vyuo 20 ambavyo vinatoa elimu ya juu na zipo sheria mbali katika vyo ambazo zimewekwa lengo ni kumlinda mwanafunzi katika kuepukana na vitendo vya udhalishaji na kufikia malengo husika aliyokusudia.
Hata katika vyuo zipo serikali za wanafunzi zikiwa na lengo la kupeleka kero na kuwasemea ama kuwakikisha wanafunzi wengine ili kuboresha mstakbali wa elimu ya juu kwa ufanisi.

WANAHARAKATI
TAMWA 

Afisa program wa maswala ya udhalishaji kutoka chama cha wandishi wa habari wanawake tanzania tamwa  Asya Hakim amesema wanachukuwa jitahada za kutosha katika kutoa elimu kwa wandishi wa habari ili kupaza sauti za wasio na sauti.
“zipo sehemu mbali mbali ambazo watoto na wanawake wanafanyiwa maswa ya udhalilishaji hivyo jamii inapaswa kuchukuwa hatua na kila mmoja ahakikishe anawajibika katika nafasi yake ili kupunguza janga hili”alisema.
Aidha alisema kuwa,ipo miradi mbali mbali ambayo wajikita katika kupambana na janga hilo hivyo jamii inatakiwa kuoa ushiriano ama ziashiria vya janga hilo.

VIONGOZI WA DINI
Dini zote zimekataza vikali vitendo vya udhalilishaji ,unyanyasaji,na ukatili wa kijinsia katika jamii.Mafundisho ya ya kidini yanaeleza jamii katika misingi ya haki ,usawa na upendo ,huku yakisisitiza kuwa vitedo hivyo vya udhalishaji utu ni dhambi na uvunjifu wa sheria za mwenzi mungu( ustadhi ali aliesema hayo.) 
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments