Asasi za kiraia Zanzibar (CSOs) zimetakiwa kujiwekea utaratibu maalumu wa kujipima kila baada ya kipindi cha miezi mitatu kwa lengo la kujitathmini na kutambua njia bora za kufikia malengo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa wakati alipokua akizungumza na baadhi ya wawakishi wa asasi 30 kutoka Unguja na Pemba katika mkutano uliofanyika kwenye umbi wa Chama hicho Tunguu wilaya ya kati Unguja.
Alisema Asasi za kiraia zina
mchango mkubwa wakuleta mabadiliko kwenye jamii, hivyo wana wajibu wa
kujiewekea utaratibu maalumu ambao utawapa fursa wahusika kujitathmini na kujua
wapi walipo na wanataka kufanya nini.
Alisema ili Asasi hizo ziweze
kuendelea kufanya kazi zao kwa maslahi ya jamii wanapaswa kuacha kufanya
kazi kwa mazoea wakiamini kuwa kila kitu ni rahisi na wataweza tu
kutimiza wajibu wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji mwevuli wa Asasi za kirai Zanzibar (ANGOZA) Mwalim Hassan Khamis Juma
alisema mkutano huo ni muhimu sana katika kupata taarifa za awali zinazohusiana
na maswala ya utetezi ambazo,zitapelekea kujua mapungufu yaliopo hatimae
kuchukuliwa hatua za kujengeana uwezo kukabiliana na mapungufu hayo.
Aliwataka washiriki wa mkutano
huo kujikita zaidi katika mambo muhimu ambayo yataorodheshwa na kisha
kujadiliana kwa pamoja ili walio mwengi zaidi waweze kufaidika.
Miongoni mwa washiriki wa
mkutano huo Maulid Sleiman kutoka (ZYF) alisema mkutano huo ni muhimu sana kwa
maslahi ya Asasi na jamii kwa ujumla.
Alisema kukutanishwa pamoja
kwa Asasi kunatengeza mahusiano mazuri sambamba na kujifunza kile ambacho
wengine wanatekeleza na kuamini kuwa ni jambo muhimu sana.
Nae Zawadi Abdalla Khamis
kutoka taasisi ya (ZGC) alisema mkutano huo utatoa mwanga na kutambua madhaifu
yao kama wawakilishi wa taasisi zao na ndio njia kuu itakayopelekea mabadiliko.
Mkutano huo wa siku moja umeitishwa na TAMWA-ZNZ
kwa kushirikiana na shirika la Foundation for Civil Society.
0 Comments