Imeandikwa na Mwandishi wetu - Zanzibar

Mwenyekiti wa “Tume Huru ya Uchaguzi ya Serikali ya Wanafunzi” wa Chuo cha Institute Of Continuing and Professional Studies (ICPS)  Ndug Hassan Haji Mwadini amesema, tume imekalisha jukumu la kusimamia matakwa ya wanafunzi  ya kupata raisi wa awamu ya kumi (10) wa chuo  na kilichobakia ni kusubiri kuapishwa kwa raisi huyo mteule  na kuanza utekelezaji wa majukumu yake.

Kauli hiyo ameitoa jana alikupokua akizungumza na mwandishi wa habri hizi aliyetaka kufahamu kuhusu mchakato wa uchaguzi ulivyokua na jinsi alivyopakana raisi mteule chuoni hapo, ambapo amesema, uchaguzi ulikua huru na wa haki na kila mgombea alipata haki yake na hakukua na masikitiko yoyote.

Akiendelea kueleza amesema, uchaguzi  ulitanguliwa na kampeni za kujinadi kwa wagombea wote wa urais na kila mmoja alitoa ahadi zake na ushawishi wake, hatimae mmoja ameibuka mshindi na anatarajiwa kuapishwa rasmi tarehe 08 June 2024  saa 4 asubuhi hapohapo chuoni  kwao Chukwani Zanzibar

“ uchaguzi haukua na chembe ya wasiwasi wala ghushi, mambo yalikua waziwazi  kwa kila mtu, na wanafunzi ambao ndio wapiga kura walijitokeza kwa wingi, na tulipohesabu kura hizo, sisi na mawakala wa wanafunzi wa wagombea, kwapamoja tulidhirika kuwa  Nd Salmin Juma Salmin amekua rais mteule kwa kuwashinda wagembea wenzake wawili katika kinyang’anyiro hicho cha uraisi wa chuo” alisema Mweyekitu huyo.

Sabah Salum Mohd wakala wa mgombea urais ndg Abrahman Rashid (Mhasibu) amesema, uchaguzi ulikwenda vizuri na hakukua na changamoto kubwa ambazo zingeathiri uchaguzi huo “ukweli tuuseme, asiekubali kushindwa si mshindani, mambo yalikwenda waziwazi na mgembea wangu alishindwa nikiwa naona, sikua na jinsi zaidi ya kukubaliana na matokeo, alisema Sabah.

 


Nae Nassra Savor, wakala wa mgembea ndg  Salmin Juma amefahamisha “nyota njema huonekana asubuhi, nilisimama katika uwakala wangu kwa uhakika wa ushindi, mgembea wangu alikua ana kila sababu, mtanashati, mtimiza ahadi na ana mawazo makubwa ya kimaendeleo ya kuwasaidia wanafunzi, kwa wote waliyomsikiliza hawakuacha kumpa kura, mana si rahisi kumsikiliza kisha usimuunge mkono, na kura alizozikosa pengine wanafunzi hao hawakuwepo siku ya kampeni” alisema Savor.

Kwaupande wake Mlezi wa Wanafunzi chuoni hapo ambae pia ni Mkufunzi katika fani ya Manunuzi (Procurement) Mr Khamis Othman Hamad amesema, wao kama chuo wameridhika na mchakato wote wa uchaguzi huku akimtakia kheri raisi mteule “kimsingi, tunamtakia kila la kheri mteule , kushinda ni jambo moja na kupiga kazi ni jambo jengine, tunamsihi akawasaidie wenzake na chuo kwa ujumla, kwakua ameshapita nasi tunamuamini” mwisho wa kunukuu.

Jumamosi  ya tarehe 08 June mwaka huu, katika viunga vya chuo cha ICPS  ndio siku inayoratajiwa kufanyika sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Nd Salmin Juma Salmin baada ya kushinda kwa ushindi wa 64% dhidi ya wapinzani wake ndg Ibrahim Mohd Haji aliyepata 6% ya kura na Ndugu Abrahman Rashid Mhasibu ambae alipata 28% ya kura hizo, jumla ya  kura zote zilizopigwa na 348

Sherehe za kuapishwa raisi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho zitahudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo kutoka Serikalini (SMZ) taasisi binafsi na wananchi wa kawaida.

Chuo cha Institute Of Continuing and Professional Studies (ICPS)  kipo Chukwani  Zanzibar na kinasomesha masomo tofauti  kwa  ngazi mambali mbali kuanzia cheti na kuendelea na kozi zinazosomeshwa ni pamoja na  Project Planning and Management, recording and achieve management, human resource management, information Communication technology, accountancy , procurement and supply , early childhood and primary education, na business operations assistant –BOA

ICPS CONTACT

+255776767494 or +255654585060