Imeandikwa na Tatu Juma – Zanzibar

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake  TAMWA Zanzibar Dkt. Mzuri Issa Ali amewataka wadau pamoja na wanaharakati wa mazingira kujenga uhusiano mzuri kwa vyombo vya habari ili kutatua changamoto zilizopo katika mabadiliko ya tabia nchi.(Climate change)

Ameyasema hayo katika kikao cha kuandaa muongozo wa namna gani waandishi watakavyo  kutoa taarifa kwa jamii kutokana na mabadiliko ya tabianchi (Climate change)  yaliyotolewa kwa waandishi wa habari kuko Ofisi ya TAMWA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema muongozo huo utasaidia kuleta mabadiliko makubwa nchini hivyo ni vyema waandishi kuitumia elimu hiyo ili kuhakikisha mabadiliko ya nchi yanabadilika kwa kiwango kikubwa."Nivyema kuufanyia kazi muongozo huu mliopatiwa kileta mabadiliko ya tabianchi kwa jamii zilizotuzunuka"alisema.

Akizungumzia kuhusu masuala ya kijinsia katika mabadiliko ya hali ya nchi aliwataka wanawake kufanya kazi kwa kujiamini sambamba na kuondoa hofu wakati wanapotoa taarifa husika kwa vyombo vya habari.

Kwaupande wake Mkufunzi wa muongozo huo Bi Shifaa Said Hassan amewataka waandishi hao pamoja na wadau wa sekta mbali mbali kufanyia kazi muongozo huo ili kuweza kujitambua pamoja na kutathmini jinsi gani ya kutumia vyombo vya habari pamoja na kusimamaimara katika kufanikisha muongozo huo.


Mkufunzi wa muongozo huo Bi Shifaa Said Hassan

Hata hivyo amesisitiza wanawake kufahamu umuhimu wa kutumia vyombo vya habari kwani ipo haja ya kujenga uimara wa kuvitumia vyombo vyombo hivyo katika kufanikisha lengo hasa la mabadiliko ya tabia ya nchi (Climate change)

Akitoa mchango katika hafla hiyo Muhandisi kutoka SUZA Dkt. Salum Suleiman Ali amesema kwa waandishi ipo haja ya kupata taaluma ya kufafanua pamoja na kuleta uhalisia wa kazi zao nakuhakikisha wanatoa mifano halisi iliyomo nchini dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.