Katika harakati za uchaguzi zinazoendelea Zanzibar mwaka 2025, sauti ya wanawake wagombea inaendelea kufifia huku wengi wao wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kifedha. Ukosefu wa ruzuku na msaada wa kampeni kutoka kwa vyama vyao au taasisi husika umekuwa kikwazo kikuu kwa wagombea wanawake wengi, hasa walioko katika kisiwa cha Pemba.
Yumna Ahmed Khalid , mgombea kupitia chama cha ADA TADEA katika Jimbo la Chambani, anasimulia kwa uchungu:
"Nilikuwa na dhamira, nguvu, na mpango thabiti wa kampeni. Lakini ukosefu wa fedha ulinifanya nishindwe kuchapisha mabango hata mawili na kuishia kuchapicha picha tuu. Nilitegemea ndugu na marafiki, lakini si kila mtu ana uwezo. Wanawake wengi tumebaki na ndoto, si ushindi."
Changamoto ya Fedha katika Kampeni za Siasa.
Changamoto hii imekuwa kikwazo sugu kwa wanawake wengi Zanzibar, licha ya kuwepo kwa sera na mikataba ya kimataifa na kitaifa inayolenga kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika siasa na uongozi.
Sheria na Mikataba Zinazounga Mkono Wanawake Kisiasa
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 (marekebisho ya 2010), kifungu cha 21(1) kinaeleza wazi haki ya kila raia kushiriki katika shughuli za kisiasa na kushika nyadhifa za uongozi. Hii ni haki ya kikatiba ambayo haiwezi kuwa ya maana ikiwa wanawake hawapati mazingira ya usawa kufanikisha kampeni zao.
Zaidi ya hapo, Sheria ya Usawa wa Jinsia (The Zanzibar Gender Policy 2016) inasisitiza kujumuishwa kwa wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi. Lakini changamoto ya rasilimali za kampeni bado haijatatuliwa kivitendo.
Katika ngazi ya kimataifa, Tanzania ikiwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa, imeridhia mikataba kadhaa kama: -Mkataba wa Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW, 1979) - Mpango wa Beijing wa mwaka 1995 (Beijing Platform for Action) - Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hususan lengo namba 5: Usawa wa kijinsia
Hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa utekelezaji wa mikataba hii unakwama katika hatua ya vitendo, hususan linapokuja suala la kutoa ruzuku au msaada wa kifedha kwa wagombea wanawake.
Vyama vya siasa vyatupiwa lawama
Ingawa vyama hupokea ruzuku kutoka serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wanawake wengi wanasema hawana sauti katika matumizi ya fedha hizo. Asha Saidi Suleiman mgombea wa chama cha Ada Tadea Katika Jimbo la Mtambile kisiwani Pemba, anasema:
"Nilipokwenda kuuliza kama nitapewa msaada wa mafuta na mabango, waliniambia nitumie juhudi binafsi kwanza. Lakini juhudi bila pesa hazisaidii."
"Wanawake ni kundi maalum na kwa miaka mingi limeachwa nyuma hivyo lazima vyama wive vina sera ya kijinsia na kuzitekeleza ili kumkomboa mwanamke "Alisema Dk Mzuri Issa Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa Habari Tanzania (Tamwa-Zanz).
Matokeo yake ni kushindwa kabla ya ushindani
Wagombea wanawake wanashindwa kufanya mikutano ya kampeni yenye hadhira kubwa, Kutangaza sera kupitia vyombo vya Habari, Kuwafikia wapiga kura vijijini
’’ Kwa kweli, serikali haikutoa ruzuku ya moja kwa moja kwa ajili ya kampeni , lakini sisi kama wanachama wa chama tulijipanga na kujichangisha kupitia harambee ili kuhakikisha tunapata angalau msaada wa mafuta na mabango ya kampeni."
Kauli hii ikionyesha juhudi binafsi za wanachama wa vyama vya siasa, licha ya kutokuwepo kwa msaada rasmi wa kifedha kutoka serikalini.
Mashirika ya kiraia yahimiza mabadiliko
Kwa mujibu wa Ripoti ya TAMWA-Zanzibar (2021), zaidi ya asilimia 70 ya wagombea wanawake walikiri kuwa ukosefu wa fedha ulikuwa sababu kuu ya kushindwa kufanya kampeni kwa ufanisi.
Wengi wao walitegemea michango midogo ya kifamilia, wakati wagombea wanaume walipata misaada mikubwa ya kifedha kutoka kwa wafanyabiashara, marafiki au ndani ya vyama vyao.
Ripoti hiyo inaeleza kwamba baadhi ya wagombea wanawake walishindwa kufika vijiji vyote katika majimbo yao, wengine walishindwa kulipa mawakala, na baadhi walitumia njia za uhamasishaji za jadi kama mikutano midogo au nyumba kwa nyumba, ambazo hazikuwa na athari kubwa kwa wapiga kura.
Mgombea wa nafasi ya uwakilishi kupitia chama cha CUF jimbo la Mtambile Asha Siasa Ame anasema kuwa mapambano yake ya kutafuta kura yalikuwa ni makubwa lakini ukosefu wa fedha ulipunguza nguvu ya kupiga kampeni jimboni.
Pia katika ripoti ya TAMWA ya mwaka 2024, ilibainishwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagombea wanawake hawakupokea msaada wowote wa kifedha. Hali hii iliathiri uwezo wao wa kushindana na wanaume.
Uhusiano Kati ya Ukosefu wa Ruzuku na Usawa wa Kijinsia
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC, 2020), vyama vingi vya siasa havina utaratibu maalumu wa kutoa ruzuku au kugawa rasilimali kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Hii inamaanisha kuwa wanawake hawapati fursa sawa za kifedha ndani ya vyama vyao vya kisiasa.
Zaidi ya hapo, tafiti za Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA) zinaonyesha kuwa baadhi ya wagombea wanawake huogopa hata kuomba msaada wa kifedha.
Hofu yao kubwa ni kuonekana “wanategemea huruma,” jambo linaloonesha athari za kijamii na kitamaduni zinazozuia ushiriki wao.
Kwa hivyo, ukosefu wa ruzuku hauathiri tu kampeni, bali unadumisha mfumo wa kisiasa usio na usawa, unaowapa wanaume nafasi ya kuendelea kutawala vyombo vya maamuzi.
Kaimu mratib Tamwa Zanzibar kwa upande wa Pemba Amina Ahmed Moh’d anasema juhudi ambazo zinachukuliwa na chama hicho ni kuhakikisha wanawake hao wanapaza sauti zao na kuzisemea chanagamoto zinazowakumba katika harakati mbalimbali ikiwemo za uchaguzi.
Athari za Kijamii na Kisiasa
Ukosefu wa ruzuku kwa wagombea wanawake una madhara ya muda mrefu kwa Zanzibar, hasa katika maeneo matatu muhimu ikiwemo kupungua kwa uwakilishi wanawake katika vyombo vya maamuzi.
Kwa mujibu wa takwimu za ZEC mwaka 2020, idadi ya wanawake walioingia Baraza la Wawakilishi haikuzidi asilimia 15, licha ya jitihada za serikali kupitia viti maalum.
Hii ni dalili kwamba mfumo wa kisiasa bado haujawa rafiki kwa wanawake wagombea wa moja kwa moja.
Mitazamo ya Wadau na Wachambuzi
Mwenyekiti wa TAMWA-Zanzibar, Asha Abdi anasema wagombea wanawake pamoja na kuhitaji maneno ya kutia moyo, bali wanahitaji msaada halisi wa kifedha kwani bila fedha, hata sera nzuri hazitawafikia wapiga kura.
Anasema vyama vya siasa visijiweke nyuma badala yake vijiwezeshe ili kuhakikisha vinawasaidia wanawake hasa ukizingatia ni jukumu lao kuwalea ,kuwasapoti katika harakati za kugombea.
Kwa upande mwingine, UN Women Tanzania kupitia mpango wake wa Women in Political Participation (WiPP), imependekeza serikali ya Zanzibar na vyama vya siasa kuweka utaratibu wa mfuko wa usaidizi wa kifedha kwa wagombea wanawake, kama sehemu ya jitihada za kuleta usawa wa kisiasa.
Mapendekezo ya Kitaalamu
Ili kuimarisha nafasi ya wanawake katika siasa za Zanzibar, wachambuzi wa kisiasa na taasisi za kijinsia wanapendekeza hatua ikiwemo kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa ruzuku kwa wagombea wanawake.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi na wadau kama UN Women, iweke utaratibu wa kisheria wa kutoa ruzuku ndogo kwa wagombea wanawake wanaojitegemea au kupitia vyama vya siasa.
Vyama vya siasa kutunga kanuni za usawa wa kijinsia katika mgao wa fedha, kila chama kipokee ruzuku ya serikali kwa masharti kwamba sehemu yake inatengwa kwa wagombea wanawake na vijana.
Katibu Mkuu Taifa wa chama cha UDP Juma Khamis Faki anasema kupitia chama hicho wanajitahidi kuwashirikisha wanawake katika shughuli mbalimbali isipokuwa suala la ruzuku anasema si la chama badala yake ni la serikali amabayo iko madara Mitazamo ya Wadau na Wachambuzi
Mwenyekiti wa TAMWA-Zanzibar, Asha Abdi anasema wagombea wanawake pamoja na kuhitaji maneno ya kutia moyo, bali wanahitaji msaada halisi wa kifedha kwani bila fedha, hata sera nzuri hazitawafikia wapiga kura.
Anasema vyama vya siasa visijiweke nyuma badala yake vijiwezeshe ili kuhakikisha vinawasaidia wanawake hasa ukizingatia ni jukumu lao kuwalea ,kuwasapoti katika harakati za kugombea.
Kwa upande mwingine, UN Women Tanzania kupitia mpango wake wa Women in Political Participation (WiPP), imependekeza serikali ya Zanzibar na vyama vya siasa kuweka utaratibu wa mfuko wa usaidizi wa kifedha kwa wagombea wanawake, kama sehemu ya jitihada za kuleta usawa wa kisiasa.
Mapendekezo ya Kitaalamu
Ili kuimarisha nafasi ya wanawake katika siasa za Zanzibar, wachambuzi wa kisiasa na taasisi za kijinsia wanapendekeza hatua ikiwemo kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa ruzuku kwa wagombea wanawake.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi na wadau kama UN Women, iweke utaratibu wa kisheria wa kutoa ruzuku ndogo kwa wagombea wanawake wanaojitegemea au kupitia vyama vya siasa.
Vyama vya siasa kutunga kanuni za usawa wa kijinsia katika mgao wa fedha, kila chama kipokee ruzuku ya serikali kwa masharti kwamba sehemu yake inatengwa kwa wagombea wanawake na vijana.
Kutoa mafunzo ya usimamizi wa fedha na ujasiriamali wa kisiasa, wanawake wanaojitosa katika siasa wapewe elimu ya kupanga bajeti za kampeni, kuvutia wafadhili, na kutumia mbinu bunifu za mawasiliano.
Kuhamasisha jamii kuondoa mitazamo hasi, jamii ifundishwe kuona wanawake kama viongozi kamili, si “wapambanaji wa muda.” Vyombo vya habari vizingatie uwiano wa kijinsia katika taarifa za kampeni na mahojiano ya kisiasa.
Katibu Mkuu Taifa wa chama cha UDP Juma Khamis Faki anasema kupitia chama hicho wanajitahidi kuwashirikisha wanawake katika shughuli mbalimbali isipokuwa suala la ruzuku anasema si la chama badala yake ni la serikali amabayo iko madarani kupitia tume ya uchaguzi.
Hitimisho
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, suala la usawa wa kijinsia linahitaji zaidi ya kauli za kisiasa. Linahitaji utekelezaji wa sera na sheria, pamoja na uwekezaji wa moja kwa moja kwa wanawake waliothubutu kugombea. Bila ruzuku ya uhakika, wanawake wengi wataendelea kushindwa, si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawakuwezeshwa kufanikisha ndoto zao.
0 Comments