Wataalamu wa maendeleo ya watoto wameeleza kuwa takribani asilimia 90% ya ukuaji wa ubongo wa binadamu hukamilika kabla mtoto hajafikisha umri wa miaka mitano, Hali hiyo inaonesha kuwa miaka ya mwanzo ya maisha ni kipindi muhimu sana kwa ukuaji wa uwezo wa mtoto wa kujifunza na kufanikiwa shuleni.
Aidha wataalamu hawa wanaeleza kuwa kumuongoza mtoto wakati yupo katika kipindi cha mwanzo cha ukuwaji ni bora kuliko kumtengeneza mtumzima ambaye tayari muda wake wamakuzi umepita, hii inamaana kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ukuwaji ni muhimu kwa mtoto kupata elimu kabla ya makazi ya utuuzima.
Kutokana na hali hiyo, wazazi, walezi na serikali kwa ujumla huhimiza watoto kupatiwa elimu wakati wakiwa katika umri mdogoilikupata msingi wa elimu wa kumjenga kimaisha kuania utotoni mpaka ukubwani.
Katika kipindi hiki mtoto hujenga uwezo wa kufikiri, kuwasiliana, kujiamini, kushirikiana na kuelewa mazingira yanayomzunguka katika jamii jambo ambala huwafanya watoto kuwa na uwezo mkubwa wakufikiri.
Wataalamu wa Maendeleo ya Mtoto ya awali (Early Childhood Development ECD) wanaeleza kuwa hatua ya awali ya ukuwaji wa mtoto ndiyo msingi unaoweza kuamua namna atakavyokua kielimu, na kukua kifikira kulingana na uwezo alionao.
Serikli ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Serayake ya elimu inawataka watoto wote wenye umri chini ya miaka ya saba kuanza nasari au elimu ya msingi kabla ya kuanza elimu ya msingi kwa lengo la kumjenga kiakili na kumpa maandalizi ya kuanza darasa la kwanza wakati anapofikia darasa la kwanza.
Aidha Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Bara la Mpinduzi Dkta Hussein Ali Mwinyi amekuwa msatari mbali wa mbele katika kuhakikisha kila mototo na wa Zanzibar wote wanapata haki yakupata elimu kwa kuwajengea mazingira ya miundombindu ya Skuli mbalimbali kote unguja na Pemba zikiwemo za horofa na Zakawaida.
Ingawa Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu na kwakua elimu ni haki ya lazima na ni haki ya msingi ya kila binaadamu lakini bado inaonekana kua changamoto kwa baadhi ya maeneo kuona kwamba mpaka sasa wananchi na watoto wanakosa haki hii muhimu maishani mwao.
Kijiji cha Kidemeni, kilichopo ndani ya Shehia ya Kwale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, sula la kutafuta elimu bado linazua maswali maswali kuhusu namna watoto wa maeneo hayo wanayopitia katika suala zima la kutafuta elimu hasa kwa watoto wanaoanza elimu ya msingi na nasari kutokana na ukosefu wa skuli kua mbali na uhaba wa vyumba vya kusomea.
Katika kijiji hicho, watoto wenye umri chini ya miaka minne wanaoanza elimu ya maandalizi hawana jengo maalumu kusomea badala yake, wanatumia ukumbi wa nyumba ya udongo uliogeuzwa kuwa eneo la kujifunzia.
Kwa kuwa wazee wengi wamebeba matumaini ya watoto wao kupata elimu, lakini pia ni alama ya changamoto inayowakabili wananchi kupata huduma hiyo ikitolewa katika mazingira bora zaidi.
Ndani ya ukumbi ule kulikua na mwanga hafifu uliokua unaingia kupitia Tundu ndogo za madirisha huku watoto Zaidi ya 76 walikuwa wakiendelea na masomo yao katika mazingira ambayo yanaonesha tofauti kubwa kati ya mahitaji ya mtoto mdogo na sehemu wanayotumia kupata elimu.
Shemsa Saidi, mmoja wa wazazi wa watoto hao,alieleza kua kumekua na changamoto ya vyumba vya madrasa ya kuweka watoto kujifunza jambo ambalo limekua likirejesha nyuma jitihada za wazazzi katika kupigania mahitaji ya watoto na kuona wanakua katika mazingira halisi ya kupata elimu na ya kujifunzia.
"Njoo uone hali halisi wanayosoma watoto wetu, Tunataka watu wajue changamoto tulizonazo ili na sisi tuonekane na tupatiwe huduma zinazostahili," aliongeza kwa kusema na kutoa msisitizo.
Kwa Shemsa, suala hili si kuhusu jengo pekee, kuhusu watoto wadogo ambao wanahitaji kuanza maisha yao ya elimu katika mazingira yatakayowapa nafasi ya kujifunza vizuri.
Mohd Rashid, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, anasema jamii imejikuta ikitumia nyumba ya mtu binafsi badala ya skuli iliyojengwa na serikali, jamii hiyo kwa sababu hawakuwa na chaguo jingine.
Anasema hata mwenye nyumba anayetoa eneo hilo kwa ajili ya watoto anakutana na changamoto kwa sababu sehemu hiyo bado ni makazi yake binafsi.
"Hata mwenye nyumba anapata shida, lakini hana jinsi kwa sababu anaona watoto wanahitaji kusoma. Tunavumilia kwa sababu hatuna sehemu nyingine," alisema.
Kwa wazazi wa Kidemeni, wanachotafuta si upendeleo, bali wanahitaji watoto wao waanze safari ya elimu wakiwa katika mazingira yanayothamini umri wao na mahitaji yao.
kuna usemi wa Kiswahili kua elimu niufunguo wa maisha lakini kwa watoto wakijiji hiki jambo hili bado linasalia kua ni ndoto inayo tembea bila kufikiwa hivyo mamlaka husika lazima kuangalia namna bora yakumsadia mtoto huyu kupata elimu, zaidi ya yote, anahitaji nafasi ya kuamini kuwa ndoto zake zinaweza kutimia.
Nilipofika Kidemeni, nilikutana na wazazi waliokuwa na hamu ya kuonesha hali halisi wanayopitia watoto wao, Miongoni mwao walisisitiza umuhimu wa watu kufika na kujionea mazingira ya watoto wao wanatumia kila siku kupata elimu ya mwanzo.
Kutokana na nafasi kuwa ndogo, baadhi ya watoto hulazimika kukaa nje wakati wenzao wakiwa ndani ili kuendelea kufuatilia masomo, Kwa wazazi, hali hiyo imekuwa ikiwapa hofu kwa sababu wanatambua kuwa miaka ya mwanzo ya mtoto ndiyo kipindi muhimu zaidi cha kujenga uwezo wa kujifunza na kujiamini.
Tafiti mbalimbali za maendeleo ya mtoto ya awali kutoka taasisi kama Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) zinaeleza kuwa ECD haihusiani na mtoto kujifunza kusoma na kuandika pekee, bali inahusisha ukuaji wa akili, afya, hisia, ulinzi na uwezo wa mtoto kuhusiana na watu wengine katika jamii.
Hivyo, mazingira anayopatikana mtoto wakati wa kujifunza yana mchango mkubwa katika namna anavyokua na kujiandaa kwa hatua zinazofuata za elimu.
Na katika kijiji hicho, msingi huo wa ndoto unaendelea kujengwa ndani ya nyumba ya udongo huku wazazi wakiendelea kusubiri siku ambayo watoto wao wataanza safari hiyo katika mazingira yanayolingana na umuhimu wa miaka yao ya mwanzo,
Wazazi wa Kidemeni, suala la mazingira wanayotumia watoto wao kujifunzia limekuwa zaidi ya changamoto ya miundombinu wanaliona kama jambo linalogusa moja kwa moja namna watoto wao wanavyokua, wanavyojenga uwezo wa kujifunza na namna watakavyokuwa katika hatua zinazofuata za maisha yao.
Zuwena Omar ni mmoja wa wazazi wanaoishi na hali hiyo kila siku, anasema pamoja na kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao, wanabaki na hofu kutokana na mazingira ambayo watoto hao wanalazimika kutumia kwa masomo yao ya mwanzo.
Anasema mwanga hafifu ndani ya eneo hilo ni miongoni mwa changamoto kubwa wanazoziona wazazi, hasa kwa watoto wadogo ambao bado wako katika hatua ya kujenga uwezo wao wa kuona na kujifunza.
"Hatujui tufanye nini, tunajua kabisa eneo hili halitoshelezi kwa watoto wetu, lakini hatuna sehemu nyingine, tukisema tunahitaji huduma zaidi wakati mwingine tunaambiwa idadi ya watu ni ndogo au umbali haukidhi mipango iliyowekwa," anasema Zuwena.
Hata hivyo Zuwena alisema, wazazi wanaomba mamlaka husika na wadau wa maendeleo kutazama hali halisi ya mazingira wanayoishi badala ya kuangalia takwimu pekee.
Anasema hata jamii yenye idadi ndogo ya watu ina watoto wanaostahili kupata malezi na elimu bora kwa sababu haki ya mtoto haipaswi kupimwa kwa idadi ya watu wanaoishi eneo fulani.
Kauli hiyo inaungwa mkono na Maryam Nassor, ambaye anaamini kuwa watoto wa Kidemeni wana ndoto kubwa kama watoto wengine wa maeneo mbalimbali.
Anasema kukosekana kwa mazingira bora ya elimu ya awali kunaweza kuathiri mwanzo wa safari ya watoto hao ambao baadaye wanatarajiwa kuwa wataalamu katika jamii.
"Watoto hawa ndio watakaokuja kuwa madaktari, walimu, viongozi na wataalamu wengine, tunahitaji kuwajengea msingi mzuri tangu wakiwa wadogo," anasema Maryam.
Ikiwa mtazamo wa kitaalamu, elimu ya awali haipaswi kuangaliwa kama hatua ya kusubiri kabla ya mtoto kuanza elimu rasmi, bali ni sehemu muhimu ya malezi inayomwandaa mtoto kimwili, kiakili, kijamii na kihisia.
Ndiyo maana mazingira ya kujifunzia yanasisitizwa kuwa sehemu ya mchakato huo, Mtoto anayejifunza katika mazingira salama, yenye mwanga wa kutosha, nafasi ya kucheza na vifaa vinavyomfaa huwa na nafasi kubwa ya kukuza uwezo wake kwa ufanisi zaidi.
Katika Kidemeni, changamoto ya nyumba hiyo ya udongo imefanya jamii kuanza kuuliza maswali kuhusu namna huduma za maendeleo zinavyoweza kuwafikia watoto wanaoishi katika maeneo ya vijijini na yenye mazingira magumu.
Sheha wa shehia ya kwale khamis Suleiman ali alikiri kuwa kijiji cha kidemeni kinachangamoto hio ya ukosefu wa darasa.
"wazazi wameazima nyumba kwa mtu tuu na hadi sasa ameshaleta malalmiko kwangu kama sheha kua anahitaji nyumba kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ndani humo kwani hakukai familia moja
Changamoto hizi nilishazifikisha kwa viongozi serekalini akiwemo mkuu wa wilaya na uongozi wa elimu akiwemo afisa elimu mkoa katika kuona linatatuka lakini tunajitahidi kufuatilia ili kuona watoto wanapata haki hii ya kusoma eneo ambalo ni rasmi na wazazi wao wanakua salama pia na kuondokana na hofu ya kila siku alieleza sheha huyo.
Ali khamis Ali ni mwanafunzi wa skuli ya Uzalendo iliopo Gombani akielezea changmoto hio amesema kuwa anaumizwa kuona wadogo zao wanasoma katika nyumba ya udongo na ni ya mtu ikiwa wao wanasoma kwenye skuli .
Alisema pia hata yeye ambae ni kubwa na ni mtoto wa kiume hafurahishwi kutembea masafa marefu kwa ajili ya kwenda kutafuta elimu lakini anatembea kutokana na kwamba ameshazoea na ni suala la kutafuta elimu hivyo kuiomba serekali hili swala la elimu waliangalie kwa kina na kuwanusuru ndugu zao na kadhia hio ya kielimu.
Kwa wazazi, hawapuuzi juhudi zinazofanyika katika sekta ya elimu, Wanatambua kuwa walimu wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu licha ya mazingira yaliyopo, Lakini wanaamini kuwa juhudi hizo zinahitaji kuungwa mkono na uwepo wa miundombinu inayolingana na mahitaji ya watoto.
Wanasema mwalimu anaweza kuwa na uwezo na vifaa vya kufundishia, lakini mazingira yasiyofaa yanaweza kuwa kikwazo katika kufikia matokeo yanayotarajiwa.
Mohd Ali Faki ambae ni mmiliki mwenye nyumba hio amesema inafika miaka mitano amekua akitoa eneo la nyumba yake kwa wanafunzi hao kuweza kujipatia elimu lakini kwa sasa nyumba yake haitoshelezi kwani familia imeongezeka , amesema amekua akishindwa kupumzika kutokana na kelele za watoto ikiwemo kufanya uharibifu kwa kufukua huku ikiwa ni ya udongo .
Ameiomba serekali kuingiza mkono wake kuwajengea kwa haraka nassary wanafunzi hao kwani hata yeye anapitia changamoto kuwepo kwa wanafunzi hao hapo nyumbani
Khamis Faki Ibrahim ameeleza kuwa kukosekana kwa darasa imekua ikiwasumbua hata wao wazazi kwani wanalazimika kuongeza mahitaji ikiwemo kufua na kukata sare mara kwa mara kutokana na watoto kujichafua Zaidi katika nyumba hio ya udongo
Nurhat kassim khamis amesema kuwa nyumba hio ina familia 3 haitoshelezi kuweza kutumia wao na wanafunzi wote wa kijiji kutokana na udogo wake hivyo kuiomba serekali kuliona hilo kwani wenye nyumba wamekua wakisema kuwa itafika mda kusitisha huduma hio kutokana na ufinyu wa eneo lao
Mwalimu wa wanafunzi hao ambae ndio mwanzilishi wa skuli hio amesema kuwa awali walianza na wanafunzi 150 na hadi sasa ana idadi ya wanafunzi 76 ambao wanaendelea klupata elimu kupitia nyumba hio ndogo ya udongo
Amesema serekali ina uwezo wa kujenga hivyo itekeleze hilo ombi ili kuondoa changamoto hio .
Amesema watoto wamekua wakikataa kufika darasani na kudai kuwa sio skuli kutokana na mazingira yaliopo ambapo pia wanalazimika kuja saa mbili kutokana na kua ni nyumba na wenye nyumba bado hawajaamka na kuhamisha vitu vyao.
“Wazazi wanajitahidi sana kuwahimiza watoto wao kufika hapa mapema lakini watoto baadhi yao wamekua wakikataa kutokana na kwamba hio sio eneo rasmi la kusomea sio skuli ni nyumba ya udongo”
“Mimi nishahama kwenye hii nyumba lakini wenzangu wamo nikisema nakuja mapema nalazimika kukaa nje na wanafunzi mpaka waamke wakunje mikeka magodoro,viatu ndio tupate sehemu tusafishe tuweze kusomea, mimi najua kabisa kua nakera wenzangu lakini changmoto hizi zinatukwaza kwenye ufundishaji.
Baada ya kilio cha wazazi wa Kidemeni kuhusu mazingira ambayo watoto wao wanatumia kupata elimu ya awali kufika kwa mamlaka husika, hatua iliyofuata ilikuwa kutafuta majibu kuhusu hali hiyo na kujua ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa ili kuhakikisha watoto hao wanapata mazingira bora zaidi yanayozingatia mahitaji yao ya ukuaji.
Changamoto hiyo pia ilimfanya Afisa Elimu Mkoa wa kusini Pemba, Mwalimu Mohd Shamte, kufika katika eneo hilo baada ya taarifa za hali hiyo kufika kwake.
Baada ya kutembelea eneo hilo na kuona mazingira ambayo watoto hao wanatumia kama darasa, alikiri kuwa hali hiyo haikidhi mahitaji ya watoto wa elimu ya awali alisema tatizo siyo tu ukosefu wa jengo, bali pia mazingira yenyewe hayajaandaliwa kwa ajili ya kumlea na kumkuza mtoto katika hatua hiyo muhimu ya maisha
Mwalimu Shamte, anaeleza kuwa changamoto kubwa aliyoiona siyo tu ukosefu wa jengo maalumu la darasa, bali pia mazingira yenyewe ambayo hayakuandaliwa kwa ajili ya watoto wadogo wanaohitaji nafasi salama ya kujifunza, kucheza na kujenga uwezo wao wa awali, alieleza.
Aliendelea kusema kuwa kwasasa chumba kinachotumika kama darasa ni sehemu ya nyumba ya mtu binafsi, jambo ambalo limefikia hatua ya kuathiri matumizi ya kawaida ya nyumba hiyo.
‘’wakati mwingine watoto hulazimika kusubiri shughuli za familia inayomiliki nyumba hiyo kumalizika ndipo waanze masomo yao, hali ambayo inaonesha ukubwa wa changamoto inayowakabili watoto hao katika kupata mazingira yanayofaa kwa elimu yao ya mwanzo.
"Mazingira yale hayaridhishi hata kidogo kwa watoto wa umri huo, nilifika na kuona hali halisi, chumba wanachotumia ni sehemu ya nyumba ya mtu na hata mwanga ni hafifu, Pia kuna changamoto ya moshi unaoweza kuwaathiri watoto kutokana na ukaribu wa eneo la mapishi," alisema Mwalimu Shamte.
Alisema hatua ya kwanza ambayo imeanza kuchukuliwa ni kuwataka wananchi wa Kidemeni kutafuta eneo ambalo wanaweza kulikabidhi kwa ajili ya ujenzi wa eneo maalumu la kujifunzia watoto hao.
Alisema upatikanaji wa eneo hilo utakuwa mwanzo wa hatua nyingine ambazo zitasaidia kuboresha mazingira ya elimu ya awali katika kijiji hicho.
Mwalimu Shamte alisema serikali inaendelea kuunga mkono upatikanaji wa elimu katika maeneo yote, ikiwemo kuhakikisha walimu na vifaa vya kufundishia vinapatikana hata katika maeneo yenye changamoto za miundombinu.
Alieleza kuwa juhudi hizo zinaonesha dhamira ya kuhakikisha watoto wanapata fursa ya elimu bila kujali wanaishi katika mazingira gani.
Aidha, alisema endapo wananchi watakubaliana na kupatikana eneo la kujenga, kuna mpango wa kuangalia uwezekano wa kuweka madarasa zaidi katika eneo hilo ili kupunguza changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Hatua hiyo ina umuhimu mkubwa kwa sababu elimu ya awali siyo tu maandalizi ya mtoto kuelekea shule ya msingi, bali ni sehemu ya malezi na makuzi yanayomjenga mtoto kimwili, kiakili, kihisia na kijamii.
Wataalamu wa maendeleo ya mtoto wanaeleza kuwa mazingira ambayo mtoto anakulia na kujifunzia yanaweza kuwa na athari kubwa katika uwezo wake wa kujifunza na kujiamini katika hatua zinazofuata za maisha.
Kwa msingi huo, changamoto ya Kidemeni inagusa zaidi ya ukosefu wa jengo, Inagusa haki ya mtoto kupata mazingira yatakayomsaidia kukua na kufikia uwezo wake kamili.
Sheria ya Mtoto Zanzibar Na. 6 ya mwaka 2011 inaweka msisitizo katika kulinda maslahi bora ya mtoto na kuhakikisha anapata huduma zinazohitajika kwa maendeleo yake, huku Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto ukitambua umuhimu wa mtoto kupata ulinzi, elimu na mazingira yanayomuwezesha kukua vizuri.
Kwa wazazi wa Kidemeni, kauli ya serikali imewapa matumaini mapya, lakini bado wanangoja kuona hatua hizo zikigeuka kuwa matokeo yatakayobadilisha maisha ya watoto wao.
Wanatambua kuwa walimu wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika mazingira magumu, lakini wanaamini kuwa juhudi hizo zinahitaji kuungwa mkono na uwepo wa miundombinu inayolingana na umuhimu wa elimu ya awali.
Kwao, nyumba ya udongo iliyogeuzwa kuwa darasa imekuwa ushahidi wa juhudi za jamii kuhakikisha watoto hawakosi elimu, lakini pia ni ukumbusho wa kazi iliyobaki kuhakikisha kila mtoto anaanza safari yake ya elimu katika mazingira yanayolinda afya, usalama na ndoto zake.
Elimu niu funguo wa maisha usemi huu utaakisi pale tu jamii ya watu wa kidemeni wakiona kua tayari na watoto wao wamepata eneo na mazingira mazuri ya watoto wao kujifunzia na kupata elimu iliyo bora.
Hivyo ni wazi kua jamii husika pamoja na jitahada za wazazi kwa watoto wao ni vyema mamlaka husika wizara ya elimu, ofisi ya wilaya mkoa na wilaya na wadau wengine wa elimu kuona kuwa ipo haja watoto hao wanapata haki yao ya msingi kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu .
‘’ Henry Ford aliwahi kusema kuwa ‘’(Anyone who stops learning is old, whether at twenty or eighty) Anyone who keeps learning stays young.” akiwa na maana kuwa mtu yeyote anayeacha kujifunza ni mzee, awe na umri wa miaka ishirini au themanini, mtu yeyote anayeendelea kujifunza hubaki kijana.
0 Comments