Imeandikwa na Fatma Abrahman - Pemba 

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Dokta Salim Ahmed Salim Kisiwani Pemba wametakiwa kujiepusha na vitendo vya Udhalilishaji na Utumiaji wa dawa kulevya ili kufikia malengo waliojiwekea.

Akitoa elimu ya msaada wa kisheria Kwa wanafunzi hao msaidizi wa Sheria Shehia ya Wawi Haji Nassor Mohammed, amesema tafiti zinaonesha waathirika wakuu wa vitendo vya Udhalilishaji ikiwemo Ubakaji, Ulawiti na Ukatili wa Kijinsia ni wanafunzi Skuli za msingi na Sekondari.
Aidha amewasihi wanafunzi hao kuwatumia Wasaidizi wa Sheria ili kupata ufumbuzi juu ya changamoto mbali mbali za kisheria zinazowakabili.
Nae msaidizi wa Sheria jimbo la Wawi Bi. Fatma Hilal, amesema miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo na kutokutimiza ndoto walizojiwekea ni pamoja Utumiaji wa dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka Shehia ya Wawi na Wara Inspekta Issa Ahmada Iddi, ametaka wanafunzi hao kuachana na dhana kwamba mwanafunzi hawezi kuchukuliwa hatua za kisheria pindi anapikosea ili kuepukana na kuingia hatiani Kwa makosa mbali mbali.
Akifunga mkutano huo mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Ndugu Khamis Said Othman, amewasihi wanafunzi hao kuwa karibu zaidi na walimu wao ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kuweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Nao baadhi ya wanafunzi hao wameahidi kuifanyia kazi elimu hiyo ili kufanya vizuri katika masomo sambamba na kutimiza ndoto walizojiwekea.
Elimu hiyo ya msaada wa Kisheria juu ya Vitendo vya Udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya Kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Dokta Ahmed Salim Ahmed yametolewa na Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Chake Chake (CHAPO).
May be an image of 2 people, people studying and dais
All reactions:
Fatma Abrahaman and 10 others