Imeandikwa na Fatam Abrahman - Pemba
Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kujisajili kwa wakati katika mfuko wa huduma za Afya Zanzibar ili waweze kupata huduma ifikapo October mosi mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya usajili na Uanachama kutoka Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Ali Idrissa Abeid mara baada ya kupatiwa uwelewa Amesema Watumishi watakaopata huduma ni wale waliojisajili katika Mfumo hivyo amewataka Wanatumishi hao kujisajili mapema ili kuweza kupata huduma wakati mfuko huo utakapoanza kufanya kazi.
Aidha amesema lengo la mfuko huo ni kutoa huduma bora , rahisi na usawa kwa Wananchi wote katika maeneo yao.
Hata hivyo amewataka Watumishi hao kuhakikisha Vielelezo wanavyovipeleka vinakuwa katika hali nzuri ili kujiepusha matatizo yanayoweza ikiwemo kuchelewa kupata uduma.
Mbali na hayo amesema Serikali inakusudia kufanya tahmini maalum ili kuweza kuwabaini Wananchi wasiokuwa na uwezo na kuhakikisha wanapata huduma sawa kama watu wengine.
0 Comments