Imeandikwa na Fatma Abrahman - Pemba


- Makamu Mwenyekiti Zainab Shomari ampongeza Rais Mwinyi_
- Awataka wanawake kuongeza kasi ya uzalishaji Mwani_
Makamu mwenyekiti wa UWT Ndg Zainab Shomari (MNEC) amesema, ujenzi wa kiwanda cha Mwani Kisiwani Pemba, moja kwa moja unakwenda kuinua na kuongeza thamani ya zao hilo pamoja na kuongeza kipato cha wananchi hususan akina mama, kwakua ndio wanaoonekana mstari wa mbele katika ukulima wa zao hilo.


Zainab ameyasema hayo leo 25/2023 huko Chamanangwe Wilaya ya Wete Kaskazini Pemba wakati alipokua akitembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda hicho cha Serikali kilichogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 8 katika hatua zote za ujenzi wake.


Amesema “Serikali ya Rais Dokta Mwinyi inaendelea kuboresha viwanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza nguvu ya ukuwaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na yote yanayoendelea kufanyika ni Utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2025.

Baadhi ya wakulima wa zao la Mwani Kutoka Jimbo la Kojani Pemba wamesema, hatua ya kujengwa Kiwanda hicho imeonesha kuwa Serikali ina wajali na kuwathamini, huku wakiamini kua, uwepo wa kiwanda hicho kutaleta fursa kubwa za kiuchumi na hatimae maisha yao kubadilika.
Aidha, wamempongeza Dr Mwinyi kwa kuwaletea maendeeleo hayo na kuomba kuongezewa bei ya bidhaa hiyo ili wazidi kunufaika.
Ziara hio ambayo imefanywa na viongozi wa UWT ni katika utekelezaji wa ilani ya chama ya 20/25 ya kumpongeza Dr Husein kwa namna ana yoiongoza Serekali.