Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) imewahimiza Masheha kutoa mashirikiano ya pamoja katika zoezi la uhakiki wa majengo unaotarajiwa kufanyika kwa lengo la kujua majengo yanayohusika na ulipaji wa Kodi za majengo kwa mujibu wa sheria.
Kamishna ameyataja majengo ya makazi ambayo yatahusika kutozwa kodi na ambayo hayatatozwa Kodi ikiwemo majengo ya Ibada, shule na hospitali .
Aidha amesema kupitia agizo la raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Husein Ali Mwinyi ni kua mwaka majengo yote ya makaazi yasio ya ghorofa yamesamehewa kulipiwa Kodi .
Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba wameahidi kutoa mashirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar katika kutekeleza majukumu yaliokusudiwa .
Licha ya kutaka kupatiwa ufafanuzi wa maswali mbali mbali yanayohusiana na Kodi baadhi ya masheha wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka hiyo ili kuhakikisha zoezi linatekelezeka ipasavyo.
Elimu hio ya Kodi ya majengo imetolewa na ZRA ambae ndie wakala mkuu wa ukusanyaji wa Mapato ya Zanzibar ambapo hiyo ni utekelezaji wa Sheria ya no 14 ya mwaka 2018
0 Comments