Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar

Mkuu wa Wilaya Kaskazini "A" Bw. Othman Ali Maulid
amesema utolewaji wa Elimu ya Utambuzi wa alama za pesa pamoja na utunzaji bora wa pesa ni muhimu katika kupiga vita uingizaji wa pesa haramu nchini.
Amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Elimu ya utambuzi na utunzaji wa pesa huko katika ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja.
Amesema Wananchi hawana uelewa mkubwa katika kuzitumia alama za pesa pamoja na utunzaji hivyo inapelekea uingiaji mkubwa wa pesa haramu.
Kwaupande wake Afisa Sarafu kutoka BOT Zanzibar Ndgu Khalid khamis amesema ukosefu wa uelewa wa alama za pesa pamoja na utunzaji mbaya wa fedha unapelekea kushuka kwa uchumi wa Nchi kutokana kwa ongezeko kubwa la pesa zisizo halali.
Nae Sheha wa shehia ya matemwe Wadi Ali Wadi ametoa ushauri kwa uongozi wa BANK KUU TANZANIA kuendelea kutoa Elimu kwa jamii ilikuhakikisha wanapiga Vita wimbi kubwa la uingizwaji wa pesa zisizo halali pamoja na uchakavu wa pesa unaoweza kuepukika.