Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mh.Omar Said Shaaban amewataka wakulima wa mwani Zanzibar kuzalisha mwani kwakiasi kikubwa kwani soko la zao hilo tayari limeshafika nchini.
Wito huo ameutoa katika hafla ya utiaji saini baina ya ZASCO na NUTRISAN kwa ajili usimamizi wa kiwanda cha mwani Zanzibar uliofanyika Hotel ya Verde Wilaya ya Magharib Unguja.
Hata hivyo amesema Serikali imechukua uamuzi wakujenga kiwanda hicho kwa kuzingatia mambo mbali mbali ikiwemo kuinua uchumi wa nchi na kuengeza pato la Taifa na uwezo mkubwa wa kupata ajira.
Ameendelea kwakusema kuwa Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mh Hussen Ali Mwinyi alipoingia madarakani sera aliyoitambumbulisha ni sera ya uchumi wa buluu kwahiyo zao lamwani linakwenda sambamba na sera hiyo.
Mbali na hayo pia amesema Zanzibar imekua ikijishuhulisha nakilimo cha mwani na inakadiriwa kwa kiasi cha miaka 40 inatambulika kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa wazalishaji wa mwani duniani na imekua ikiuza mwani katika Masoko ya nchi za nje.
Wakati huohuo akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa kampuni ya mwani Zanzibar Dk.Masoud Rashid Muhammed amesema mkataba huo unalengo la kuunda kampuni itakayounda umoja kati ya ZASCO na NUTRISAN kusimamia kiwanda hicho cha mwani.
Nae Mkuu wa kikosi cha kuzuia magendo Zanzibar (KMKM) Komodoo Azan Hassan Msingiri ambae ni mkandarasi wa kiwanda hicho cha mwani amezungumza kuwa kiwanda tayari kimekamilika kulingana na makubaliano ya wizara na mamlaka ya ZASCO natayari hatua za mwisho za ujenzi zinatarajiwa kufikia ukingoni.
Kampuni ya mwani Zanzibar (ZASCO) nikampini ya Serikali iliyoanzishwa kwamujibu wa sheria ya makampuni nambari 15 ya mwaka2023.
Ni kampuni inayojitegemea na inayoendeshwa kutokana na hisa za wabia ambao ni Shirika la bandari Zanzibar (ZPC),Shirika la bima Zanzibar(ZIC),Shirika la Taifa lq biashara Zanzibar ZSTC na mfuko wa Hitachi ya jamii Zanzibar (ZSSF).
0 Comments