Imeandikwa na Tatu Juma Zanzibar
Wadau wa Takwimu za biashara na uchumi wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kukusanya takwimu sahihi ili kukuza uchumi na biashara nchini.
Hayo yameelezwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar ndugu Salum Kassim Ali katika kongamano la wadau wa biashara na uchumi lililofanyika huko ofisi ya mtakwimu mkuu Mazizini Wilaya ya Mjini Unguja.
kwakushereheka kwa pamoja siku yatakwimu Afrika kwani kila mwaka inatolewa kauli mbiu maalumu.
Hata hivyo ameishauri Serikali kushajihisha wanafunzi nchini kusoma somo la data Science kwani kukosekana kwa wasomi wa fani hiyo itapelekea hasara kubwa katika nchi pamoja kukosekana kwa takwimu sahihi.
Nae kamisaa wa sensa ya watu na makaazi ndugu Muhammad Haji Hamza amesema tàarifa za sensa zina mahusiano na biashara pamoja na fedhda hivyo wale wanaoshuhulika na biashara wanawajibu mkubwa wa kuzitumia taarifa zinazotokana na sensa kwaajili ya kupanga mipango madhabuti.
Aidha amesema nivyema ikakuwepo nguvu kazi latika uwezo wa kileambacho kinazalishwa nchini pamoja na kinachotoka nje kwakuzingatia zaidi thamani ya ununuzi kwaiyo ipohaja ya kutumia taarifa za sensa kwa ajili ya kupanga na kuzalisha data.
Hata hivyo amemuomba Mtakwimu mkuu kutoa taarifa zitakazo wasaidia wazalishaji kuzitumia na kupata taarifa ambazo zitatumika kwaajili ya kuendeleza maendeleo ya biashara na uchumi.
Nae ndugu Mashavu khamisi Omar kutoka Wizara ya kilimo akichangia mada amesema nivizuri kukakuepo mfumo wa kufatitlia na kusoma taarifa za Big data kila sehemu ili kujua data hizo zinatumika kivipi katika upana wake.
Akichangia mada ndugu Haji Weka Abdullah kutoka jumuiya ya wafayabiashara Zanzibar amesema kitendo cha makubaliano ya eneohuru la biashara Afrika ni makubaliano ya kuweza kuwa nasoko moja ambalo itawezekana kuuza bidhaa na huduma Afrika kwa urahisi.
Amesema mkataba wa makubaliano nchini na nchi nyengine lengo Lake kubwa ni kupunguza ushuru wa bidhaa wakati wa kusafirisha angalau kwa asilimia 90 kwani itakua nirahisi kwa wafanya biashara kufanya biashara zao.
Ifikapo siku ya tarehe 18 /11/2023 ni siku ya Takwimu Afrika ambayo itaadhimishwa kwa kauli mbiu isemayo ''uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la bara la Afrika (AfCFTA); mchango wa takwimu rasmin na Big data katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika jukumu la takwimu rasmi na Takwimu kubwa katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika".
Kauli mbiu hiyo inawiana na kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2023 iliyohimiza "kuharakisha utekelezaji wa AfCFTA",na inajumuisha wito wa kuboresha mifumo ya data katika bara la Afrika ili kuzalisha na kutumia takwimu rasmi za ubora wa hali ya juu na kuchangamkia fursa zitokanazo na 'big data'/ takwimu rasmi.
0 Comments