Imeandikwa na Tatu Juma Zanzibar

Wazir wa Biashara Z'bar awataka watendaji kuongeza juhudi katika tafiti.
Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar
Watendaji wa Taasisi za Serikali nchini wametakiwa kuongeza juhudi za utafiti wa Takwimu ili kuleta mafanikio nchini.
Wito hio umetolewa na Waziri wa Biashara na maendeleo ya viwanda Mh.Omar Said Shàaban katiaka maashinisho ya siku ya takwimu Afrika huko Chuo cha utalii Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja.
Ameeleza kuwa kunahitajika uhamasishaji na uweleshwaji wa wadau mbali mbali kuzitumia takwimu za biashara katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini.
Amesema Takwimu za biaahara zinaonesha kuwa mchango wa nchi Afrika kwa biashara ya dunia ni asilimia 3% tu ambapo kati ya asilimia 100% ya biashara inayofanyika baina ya nchi za Afrika ni asilimia kumi tu kwa uchambuzi wa kitakwimu ulifanywa na kikosi kazi kilichofanywa na Jamuhuri ya muungano kwaajili ya kuchambua mkataba wa AfCFTA ambao umezingatia Mapato ya ushuru.
Hata hivyo amesema tarehe 21 machi mwaka 2018 Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na nchi nyengine za umoja wa Afrika zilisaini mkataba wa uwezeshaji wa eneo huru la biashara Afrika nchini Ruwanda ,baada ya chi zaidi ya 14 kuridhia mkataba huo.
Mbali nahayo pia amesema Kila ifikapo tarehe 18 Novemba kila mwaka umoja wa Afrika huadhimisha ziku ya Takwimu Afrika na lengo kuu ni kubadillishana mawazo pamoja na kuongeza ufahamu wa TAkwimu rasmi, uzalishaji usambazaji, ufikiaji na utumiaji kwaajili ya kufanya maamuzi na kuripoti kulingana na ushahidi sahihi wa kitakwimu.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya Takwimu Balozi Amina Salum Ali amesema ipo haja ya kushirikiana kwapamoja kwa kufikisha Takwimu sahihi hii itapelekea soko kuwa kubwa pamoja na kuleta maendeleo katika eneo huru la Afrika.
Akizungumza katika hafla hiyo nae Mtakwimu mkuu wa Serikali Ndugu Salum Kassim Ali amesema kuwa takwimu ni msingi wa kila kitu kwani huwezi kuishi kuholela katika maisha bila ya kutumia takwimu zozote.

Amezungumza kuwa siku ya Takwimu Afrika inaumuhimu mkubwa kwani wamefanikiwa kutengeneza matukio mbalimbali kabla ya siku hiyo ikiwemo mkutano wa waandishi,kukutana na wastaafu,kukutana na wazee Sebleni pamoja na wagonjwa pamoja na kuandaa timu za mpira na kucheza ili kufurahika kwa pamoja.