Imeandikwa na Fatma Abrahman - Pemba

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA imetakiwa kuendelea kusimamia taasisi za Bima kuharakisha ulipaji wa fidia za majanga mbali mbali zinazowatokea wanachama waliaojiunga na mifuko hiyo
Ametoa wito huo alipokuwa akifunguwa mafunzo kwa saccosi ya walimu kisiwani Pemba yalioandaliwa na Taasisi hiyo Tibirinzi Chake Chake
Naibu kamishina wa Mamlaka hiyo zanzibar Khadija Issa Said amewataka Walimu hao kisiwani Pemba kuanzisha uwakala wa bima katika Taasisi Yao ili kujiwezesha kiuchumi.
Kwa upande wake rais wa chama Walimu zanzibar ZATU Seif Mohmmed Seif ameseme taluma hiyo ya bima kwa Walimu imeweze kuwasaidia kupata taluma hiyo kwani majango yanapotokea saccos haina uwezo wa kuweza kulipia fidia hiyo.
Akitoa neno la shukuran kwa niaba ya Walimu kutoka Taasisi ya Pemba Teacher Union Said Suleiman Ameshukuru Taasisi hiyo kwa kuwapa elimu juu ya bima mbali ambazo zitasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza kila siku katika maisha
Mafunzo hayo juu ya bima mbali mbali yamekusanya Walimu wanachama wa Saccosi ambapo katika mafunzo hayo Mada mbali mbali ikiwemo bima ya muda mrefu na muda mfupi zimewasilishwa kutoka kwa watoa wa Taasisi ya bima Jubilee Alliance Insurance