Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar

Jamii imetakiwa kuchukuwa tahadhari kubwa kutokana na ugonjwa wa maradhi ya ukimwi nchini.

Wito huo umetolewa na Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Serikari inachukua miundo mbinu mabalimbali dhidi ya kupambana na maradhi hayo kwani hivi katiburi Zanzibar pamoja na Tanzania Bara ilikua na zoezi la utafiti wa kuangalia viashiria vya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akielezea matokeo ya utafiti huo ni kwamba asilimia 4.4 ya Watanzania wanaishi na virusi vya Ukimwi ambayo ni sawa na watu milioni moja laki tano na arubaini nane elfu wanaishi na maambukizo ya virusi vya Ukimwi.
Nae Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema kuwa katika mkoa huo wa Kaskazini Unguja Ukimwi upo na ipohaja ya kuchukia tahadhari kubwa dhidi ya ugojwa huo.
Amesema kuwa mwaka 2021 hadi 2022 imethibitika kuwa wananchi kumi na nne elfu mia nne na nne wamepimwa virusi vya ukimwi na wananchi hamsini na moja walionekana kuwa na maambukizo hayo na mnamo mwaka ‪2022 -2023‬ wananchi kumi natatu elfu mia nane na nne wamepimwa virusi na wananchi thelathini nanne wameonekana na virusi vya ugonjwa huo.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa bodi ya Ukimwi Zanzibar Ali Salim Ali amesema kuwa jitihada za kuwaelimisha vijana dhidi ya VVU zimeimarizhwa zaidi pamoja na kutambua kuwa kundi hilo lipo kwenye hatari zaidi ya kuambukuzwa kutokana na tabia pamoja na mazingira yao.
Kauli mbiu ya mwaka huu 2023 inasema kuwa jamii ziwezeshwe kupambana na maradhi ya Ukimwi.
Like
Comment
Share