Zanzibar yatarajiwa kufungua kitengo cha maradhi ya moyo ili kupunguza usumbufu wa wagonjwa na kutumia gharama kubwa ya matibabu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete Dk. Peter Kisenge akizungumza na waandiahi wa habari katika hafla ya mafunzo kwa madaktari wa moyo huko Verde Wilaya ya Magharib Unguja.

 

Amesema mafunzo hayo yameweza kuwashirikisha madaktari nchini na nje ya nchi ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda,Uturuki,Ijipt,Marekani ili kuleta maendelea yanayotikana na matibabu ya ugonjwa huo.

 

Amesema wanatarajia kufungua Spitali ya magonjwa ya moyo katika maeneo ya Lumumba mjini Unguja ili kuondoa usumbufu wa wagonjwa wa maradhi hayo kuweza kupata matibabu kwa urahisi zaidi.

 

Amesema tatizo la moyo linaongezeka kilakukicha duniani kote karibu watu milioni 17.9 wanapoteza maisha kila mwaka kwasababu ya maradhi ya moyo kwani hii inasababishwa  mfumo wa maisha unavyokwenda ikiwemo uvutaji sigara,unywaji wa pombe,unne uliokithiri na kutofanya mazoezi.

 

Amefahamisha kuwa magonjwa ya moyo yanamuanza mwanadamu kidogo kidogo tangu utotoni nainapofikia miaka 40 au zaidi huweza yakajitokeza hivyo ametoa tahadhari ya kuwawekea mazingira mazuri ya vyakula watoto ili kutopelekea kupatikana kwa magonjwa hayo.

 

Ameendelea kwakusema kuwa watoto wangi wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo kutokana na wazazi kutowapa lishe bora napia kutumia vinywaji hatarishi wakiwa wajawazito.

 

Nae Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Jakaya Kikwete anasimamia taasisi ya moyo Asha Ressa Izina amesema baada ya mafunzo hayo kutakuwa na mkutano mkubwa wa madaktari hao hapo kesho tarehe 9 Febuari 2024 katika Hotel ya Golden tulip Mjini Unguja ambapo mkutano huo utazungumzia zaidi huduma za moyo katika nchi za Afrika.

 

Hata hivyo amesema mkutano huo utajumuisha mafunzo mbali mbali ambayo yatawasilishwa na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini na nje ya nchi.

 

 

Amesema matarajio wanayoyategemea katika mkutano huo ni kuona kwamba wanafanikisha kwakiasi kikubwa taaluma mbali mbali za ugonjwa wa moyo.

 

Nae Daktari bigwa katika kitengo cha upasuaji moyo watoto katika Taasisi ya Jakaya kikwete Dk.Goldin G.Sharaw amefahamisha kuwa katika ghafa hiyo kuna vipengele maalumu vitakavyoweza kuzungumziwa ikiwemo upasuaji wa moyo kwa watuwazima na mishipa ya damu napia kuzungumzia matatizo mbali mbali yanayojitokeza katika ugonjwa huo.