Kampeni hii itazinduliwa kesho tarehe 28/02/2024, saa 12 asubuhi katika viwanja vya Hospitali ya Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja katika kilele cha kambi ya Matibabu na upasuaji wa bure ya "Afya Bora, Maisha Bora" inayoendelea viwanjani hapo.
Wake wa Marais watashiriki akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Angeline Ndayubaha Ndayishimiye, Mke wa Rais wa Kenya Mama Rachel Ruto, wawakilishi kutoka Nigeria ,Angola na Afisa Mtendaji Mkuu wa OAFLAD
Aidha ,Tanzania itakuwa nchi ya 22 kati ya 54 kuzindua kampeni hii chini ya uwakilishi wa Mhe.Mama Mariam Mwinyi
0 Comments