NA, FATMA SULEIMAN-PEMBA
Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imesema itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi wa majimbo katika kuwaletea maslahi wananchi wake .
Kauli hio imetolewa na Waziri wa kilimo mifugo na umwagiliaji Mh Shamata Shaame Khamis akizungumza kwa niaba ya waziri wa elimu huko wawi ikiwa ni katika hafla ya kuwatunuku zawadi walimu na wanafunzi waliofaulu mwaka 2024-2025.
Kwa upande wake afisa mdhamini wizara ya elimu Pemba mwalimu Muhammed Nasssor Salim amesema kuwa Kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutokana na viongozi kuwapatia hamasa walimu na wanafunzi .
Nae mwakilishi wa jimbo la wawi nd Bakar Hamad Bakar akizungumza katika hafla hio amesema wameamua kutoa zawadi mbali mbali kwa walimu na wanafunzi ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi zake ambazo aliwapatia ili kuongeza hamasa na ufaulu nchini.
Katika hafla hio zawadi mbali mbali zilitolewa kwa walimu na wanafunzi ikiwa ni pamoja na mikoba , sare, calculator, na magesi kwa ajili ya walimu.
0 Comments