KAMATI ZA MIRADI YA JAMII PEMBA ZATAKIWA KUENDELEA KUSIMAMIA UTENDAJI KAZI

NA, FATMA SULEIMAN-PEMBA

Katibu tawala Mkoa wa Kusini Pemba Amour Hamad Saleh amezitaka kamati za miradi ya jamii kuendelea kusimamia utendaji kazi na matunzo ya miradi hiyo ili kuongeza ufanisi.

Ameyasema hayo huko Chake chake Pemba katika hafla ya kukabidhi vyeti Kwa kamati ya ujenzi wa Kituo Cha afya Kinyikani kupitia Mradi wa kaya za Walengwa Wilaya ya Wete.

Amesema ili kupata ufanisi wa kuwepo miradi hiyo ni wajibu Kwa wanakamati kuonesha uzalendo na upendo wa kulinda maslahi ya umma na juhudi za Serikali Yao katika kututua kero za wananchi. 

Mkurugenzi wa Uratibu TASAF kutoka makao makuu Dodoma Haika Shayo amesema mfuko huo upo katika kuendeleza juhudi za serekali za kuwakwamua wananchi kiuchumi.

Mara baada ya kupokea vyeti hivyo wanakamati hao wamesema uwepo wa mradi huo katika Kijiji chao umekuja kuondoa kero ya huduma za afya.

Post a Comment

0 Comments