Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar

Afisa Uhusiano Chuo cha Waandishi wa Habari na Mawasiliano Zanzibar Mwatima Rashid Issa amewataka Waandishi wa Habari nchini kuandaa tafiti zilizosahihi ili jamii iweze kufahamu lengo halisi lililokusudiwa.

Ameyasema hayo katika hafla ya muendelezo wa  kikao cha kuandaa muongozo wa namna gani waandishi wataweza kuripoti  taarifa  za mabadiliko ya tabia nchi (limate change) kuko Ofisi ya TAMWA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Hata hivyo, amefahamisha, waandishi lazima wajenge uwelewa wa kuyafahamu maeneo sahihi ya kimazingira ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Wakati huohuo Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Imane Duwe amesema waandishi wa habari za mabadiliko ya tabianchi nivyema wakapatiwa mafunzo ambayo yanauhalisia wajambo wanalolizungumzia ili kuweza kuandika habaŕi zitakazokuwa na mvuto na uwelewa.

Amesema kuwa muongozo huo pia utasaidia waandishi kutambua jinsi gani watapata uelewa mzuri ili waweze kuleta mrejesho sahihi watakapokwenda kufanya kazi zao.

Akichangia mada katika hafla hiyo mtaalamu kutoka taasisi ya haki sawa za kijinsia biashara za kijamii CFP Zulfa Bashir amewataka wakufunzi kuwapa mafunzo madhubuti waandishi ili waweze kusimama imara na kujiamini ambapo wanapokwenda kutenda kazi zao.

Hafla hiyo ya muongozo maalumu uliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA upande wa Zanzibar utakaowawezesha waandishi wa habari jinsi ya kuandaa habari za mabadiliko ya tabianchi imehudhuriwa na baadhi ya wakufunzi wa chuo cha habari nchini,wanaharakati kutoka taasisi mbalimbli nchini,waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wakulima kutoka kisiwa cha Uzi Unguja.