NA FATMA SULEIMAN-PEMBA
Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara katika endeo la chanoni na kujionea uharibifu wa mikarafuu hiyo iliyoteketea kwa moto.
Ameeleza kuwa mkarafuu ni uti wa mgogo wa uchumi wa zanzibar hivyo kila mwananchi anahaki ya kuilinda ili kuepukana na uharibu unaoweza kujitokeza ambao unaosababishwa na watu wasio waadilifu.
Kwa upande mkurugenzi wa mfuko wa maendeleo ya karafuu Ali Sulieman Mussa ameeleza kuwa miongoni mwa makosa yanayochukuliwa hatua kisheria katika mashamba ya mikarafu moja wapo ni pamoja na kuchimba mchanga au udongo, kuchimba mawe na kupiga tanu ya mkaa, Hata hivyo amewataka wananchi kuacha kuchoma mkaa karibu na mshamba ya mikarafuu ili kupuka uharibifu wa mikarafuu.
Nae mkurugenzi mtendaji wa jumuia ya wazalishaji wa karafuu zanzibar Abubakar Moh’d Ali amesema uchomaji wa moto katika shamba za mikarafuu ni kupelekea kuathirika na kufa kwa mikarafuu hiyo sambamba na kuwataka wakulima kuachana na tabia ya uchomaji wa moto na mkaaa katika shamba hizo ili kuhuisha zao la karafuu nchini.
''Unapochoma kitu chochote au moshi upozunguka tuu karibu na mkarafuu licha ya tanu basi umeathiri, lakini pia kuuwa mkarafuu mmoja gharama zake ni kubwa kuhuisha mpaka kukua na kufikia ulipo hivyo ni vyema kutii sheria bila ya kushurutishwa''alisema.
Mmiliki wa baadhi ya mikarafuu iliyoteketea kwa moto Moh’d Abdalla Bakar ambae pia ni mtuhumiwa wa watukio hilo amesema chanzo cha moto huo hakijajuilikana licha ya watoto wake kupiga tanu katika eneo hilo.
''Kwa kweli chanzo cha moto kahijajuulikana moja kwa moja licha ya kuwa watoto wangu ndio walikuwa wanapiga tanu ya mkaa lakini ukitizama ilipo tanu na moto ulipoanzia ni vitu tofauti''.alisema.
Nae bibi shamba kutoka wizara ya kilimo Khadija Juma Abdalla amesema kwa tathmini waliyoifanya ya moto huo, imeonyesha kuwa mikarafuu mengi yao imekufa kutokana na uchomaji moto wa tano za mkaa.
Moto huo umesababisha athari kubwa kwa mashamba ya karafuu na kupelekea kukosekana kwa pato laifa kutokana na zao hilo ambapo idadi iliokadiriwa kutofikiwa .
0 Comments