Waandishi wa Habari wameaswa kuongeza hamasa kwa jamii katika kuandika habari makala na vipindi mbali mbali vinavyohusu haki ya Afya ya uzazi hususan ni kwa wanawake na wasichana ili kuongeza usalama wa afya zao na kuendelea kuwa salama .
Wito huo umetolewa na Zaina Abdalla Mzee mratibu wa mradi wa Haki ya Afya ya Uzazi kwa Wanawake na Wasichana unaotekelezwa na TAMWA_ZANZIBAR wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri katika mkutano wa tathmini juu ya habari zinazohusu maswala ya afya ya uzazi uliofanyika katika ukumbi wa TAMWA _ZANZIBAR Makanjuni Pemba.
Amesema kuna wimbi kubwa la mabadiliko ya tabia kwa wasichana wakike na wakiume ambayo huenda yasiposemewa kupitia waandishi wa habari afya ya uzazi kwa wasichana ikaendelea kuwa hatarini na kupelekea kutokufikia malengo yao ya maendeleo hivyo ni vyema kupitia Waandishi kuitumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi Kuvunja ukimya kuhusu mabadiliko ya tabia sambamba na kuzunyumza na watoto wao hususan ni wasichana na wavulana katika kubadilisha tabia na mabadiliko ya kimwili ili kuwaepusha na Athari za mabadiliko ya tabia za mwili .
kwa upande wake Ali Mbarouk Omar mwandishi mwandamizi na mkufunzi kwa waandishi wa habari katika maswala ya Afya ya uzazi amesema kuna maswala mbali mbali yanayohusu haki ya Afya ya Uzazi bado yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya wanawake ikiwemo swala ya afya ya uzazi na maradhi yasiyopewa kipaumbele kama vile maradhi ya Pressure,Kisukari,Ganzi na mengine ambayo yamekuwa na madhara makubwa kwa jamii hususan wanawake lakini bado waandishi wamekuwa hawayasemei maswala hayo katika kazi zao za kuelimisha Jamii .
Nao baadhi ya waandishi wa habari waliojengewa uwezo kuhusu uwandishi wa maswala ya haki ya afya ya uzazi akiwemo Khaulat Rashid Pamoja na Fatma Abrahman wamesema licha ya kuendelea kuandika na kutoa taarifa kuhusu maswala mbali mbali ya Afya uzazi lakini bado ugumu wa kuwapata wataalamu wa maswala hayo kutokana na sababu mbali mbali pamoja na takwimu mbali mbali umekuwa ukirudisha nyuma jitihada za waandishi hao katika kuandika habari hizo.
Kwa upande wake muhariri kutoka Radio Jamii Micheweni Rehema Ramadhan Said Ali Masoud Kombo pamoja na Bakar Mussa Juma kutoka gazeti la Zanzibar leo wamewataka waandishi kutumia ujuzi wa kitaalamu katika kufanya ushawishi wa kupata taarifa kutoka kwa vyanzo mbali mbali sambamba na kuwasemea watendaji ikiwemo wauguzi na kuweza kupatiwa elimu katika maswala hayo ya haki ya Afya ya uzazi .
Waandishi na Wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari wameshiriki kiatika Mkutano huo wa tathmini uliaondaliwa na TAMWA_ZANZIBAR .
0 Comments