Ubovu wa Barabara Andikoni Pemba chanzo cha Maendeleo Duni.


WANANCHI wa Kijiji cha Andikoni Shehia ya Chumbageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwatengenezea barabara ili kuepukana na changamoto zinazo wakabili. 
Wakizungumza mbele ya Afisa Mdhamini wananchi hao wamesema wanakabiliwa na changomoto ya Barabra kuingilia Kijiji huko licha ya Serikali kuweka baejeti ya ujenzi wa barabra lakini bado fursa hiyo haijawafikia. 
Ali Shaka Ali amesema katika Kijiji chao hawana skuli hivyo wanafunzi hulazimika kuifuata skuli katika kijiji cha tumbini jambo ambalo ni ugumu kutokana na ubovu wa barabara  hususani kipindi  hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha. 

Amesema kutokana na changamoto hiyo wananchi wa Kijiji hicho watanedelea kuwa nyuma kimaendeleo kwani ubovu wa barabra hiyo ni chanzo cha kukwamisha maendeloe ya kijiji hicho. 

Kwa upande wake Makame Mosi ameelezea adha na vigumu wa kuzifikia hudmua za kiafya hasa kwa mama wajawazito hususani nyakati za usiku kwani hulazimika kuwabeba kwa vitanda kuwapeleka hospitali kutokana na masafa makubwa na ubovu wa barabara jambalo huhatarisha Maisha ya mama na mtoto. 

Naibu sheha wa shehia ya chumbageni Moh'd Kheri Haji amesema licha ya ubovu wa barabara kukwamisha maendeleo lakini amewataka wananchi hao kuendelea kuwa wastahamilivu kwavile serikali ipo mbioni kutatua chanagmoto hiyo. 
Afisa mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasilisno na Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi inampango wa kujenga barabra hiyo mara tu baada ya kumalizika kwa mvua zinazoendelea kunyesha. 

Amefafanua kuwa kwa hatua ya awali barabraa hiyo itajengwa kwa kifusi na baadae kuweka lami ya moto hivyo amewataka wananchi hao kuwa wastahamilivu na kutoa mashrikiano na serikali ujenzi huo utakapo anza.
Barabara ya Sisimizini Andikoni yenye urefu wa kilomita mbili ni moja ya barabara za ndani zilizomo katia mpango ujenzi wa barabara za ndani zenye urefu wa kilomita 134 kwa Pemba.

Post a Comment

0 Comments