Chama cha mapinduzi mkoa wa kusini Pemba kimetoa pongezi kwa juhudi ambazo amezionesha mwakilishi wa jimbo la ole Mh Masoud za kukijenga chama sambamba na kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa jimbo hilo
Akizungumza Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa kusini Pemba Yusuph Ali Juma amesema jimbo la ole limekitendea haki chama kwa kumchagua mwakilishi mwenye kuumwa na shida za wananchi.
Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa kusini Pemba Kajoro Peter Vyohoroka na Katibu wa siasa na uwenezi mkoa wa kusini Pemba Fat-hia Hemed Saidi wamesema katika kukiboresha chama mwakilishi amejenga na kuboresha ofisi zote za chama ndani ya jimbo hilo ikiwa ni katika kutekeleza ahadi alizoziweka kwa wananchi hivyo ni vyema kuyaenzi yale mazuri walioletewa na mwakilishi wao.
Mwenyekiti wa jimbo la ole Hassan Abdallah Ali amesema zaidi ya miaka 20 hawakuwahi kuona mafanikio ambayo wameyapata hivyo wataendelea kuzienzi juhudi zilizochukuliwa na mwakilishi za kuwaletea mabadiliko ndani ya jimbo hilo.
Amesema mwakilishi amekua akileta maendeleo bila ya kugua chama chochote hivyo kuwaomba na viongozi wengine kuiga mfano wake ili kuendelea kuleta mabadiliko disembark
Amewataka wananchi wa pemba kutokufanya makosa na kuchagua viongozi wenye mfano wa masoud katika kuwaletea maendeleo na kuleta mabadiliko katika sekta zote ikiwemo kuleta mabadiliko ya kielimu afya miundombinu ya barabara maji na hata umeme .
Katika hafla hio matawi 5 ambayo aliyajenga kuanzia foundation hadi juu amekabidhi TV na vingamuzi kila tawi pamoja na kukabidhi viti
0 Comments