Imeandikwa na Tatu Juma - Zanzibar
Chama cha waandishi wa
habari wanawake TAMWA Zanzibar kimewataka wanawake kujitokeza kwa wingi katika
kushiriki masuala ya michezo.
Wito huo umetolewa na
Bi Haura Shamte alipokua akitoa mafunzo kwa wanachama wa chama hicho juu ya
masuala ya michezo na uongozi kwa wanawake huko Ofisini kwao Tamwa Mkoa wa
Kusini Unguja.
Amesema kuwa, kwaupande
wa Zanzibar jumla ya vyama vya michezo 42 na wengi wao waliojiunga na vyama
hivyo ni wanaume wakati asilimia ndogo tu niyawanawake.
Bi Haura amewataka
wazazi kutokuwa na fikra potofu kwa watoto wao kwani nadharia hii inaonesha
kuwa wanaume pekee ndio wanaostahiki kujihusisha katika michezo.
Hata hivyo amesema kuwa
waandishi wanawake walio wengi hawandiki
habari za michezo kwa sasa ipo haja kwa waandishi pamoja na watangazaji
kuchukua hatua ya kufanya utafiti na uchambuzi juu ya suala la michezo kwa upande wa wanawake ili kufikia
hatua nzuri.
Nae Mwandishi wahabari
ambae pia ni mwanachama hai wa chama hicho ndugu Salma Said amesema kuwa ipo
haja ya kuboreshwa kwa vyama vya michezo kwa wanawake kwa kuwekewa kanuni
sahihi zisizo kiuka maadili katika jamii ili kuona wanawake wengi kujihusisha
na michezo tofauti.
Wakati huohuo
mwanachama mwengine wachama hicho ndugu Nasra Hatibu amesema kuwa wanawake
walio wengi wanagoma kujiunga na michezo kwakuona kuwa inawezekana ukatumia
muda mwingi katika kutumikia taifa pasipokuwa na maslahi mazuri yakifedha hivyo
ipo haja ya kufanyiwa utatuzi tatizo hilo ili jamii iweze kuona mafanikio
hatimae kujitokeza kwa wingi.
0 Comments