CUF WAPANIA KUKIREJESHA CHAMA KAMA KILIVYOKUA AWALI

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Husna Mohamed Abdalla amewataka wananchi  Kisiwani Pemba ambao walikuwa katika chama hicho na kuondoka kuweza  kushikiana na kurejesha makali ya chama hicho.
Katibu Mkuu  ametoa wito huo  mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba kupitia bandari ya Mkoani ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kuwasili kisiwani humo tokea kuteuliwa kushika wazifa huo.
Amesema migogoro iliyokuwa ikikiandama chama hicho na kupoteza mwelekeo imeondoshwa kwa kiasi kikubwa sasa hivyo ni wakati wa kukijenga tena ili kusimama imara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF Khamis Hamad Ibrahim amesema matumaini makubwa ya chama hicho ni kushinda uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Micheweni Haji Mbwana Haji ambaye ni Mbunge wa zamani wa jimbo hilo amewaomba wananchi wa Pemba kuungana kukiimarisha chama hicho chenye historia kubwa kwa wananchi wa Zanzibar 
Awali Katibu Mkuu wa CUF Husna Mohamed Abdalla alishiriki ufunguzi wa tawi la chama hicho Mbuyuni Wilaya ya Mkoani na kuzungumza na wanachama wa chama hicho Vikunguni Wilaya ya Chake Chake.sambamba na ziara hio kumalizika na dua.

Post a Comment

0 Comments