Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) ametoa wito kwa Viongozi na Wadau mbalimbali kuchangia na kufadhili Miradi inayolenga kuwawezesha Wanawake kiuchumi.
Makamu Zainab ametoa wito huo Leo Tarehe, 24, Mei 2025, wakati wa Hafla ya Ugawaji wa mitungi ya Gesi, Viti Mwendo kwa Walemavu, pamoja Vifaa vya Michezo kwa Wajasiriliamali Kisiwani Unguj, katika Viwanja vya Mapinduzi Square(Mnarani)
"Serikali yetu ya Zanzibar inayoongwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ilizindua muongozo wa uanzishwaji wa majukwaa na uendeshaji wa majukwaa ya Wanawake ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi,lengo likiwa ni kunyanyua uchumi wa Mwanamke na kila mwananchi"
"Hafla hii ya ugawaji wa Mitungi ya gesi kwa wajasiriamali ni moja ya hatua kubwa ya kuunga mkomo dhamira ya Serikali ya Matumizi ya Nishati Safi na Salama, Na kwa kipekee nimpongeze Muwakilishi wa Viti Maalum Mhe. Tabia Mwita kwa kuratibu mpango huu na nitoe wito kwa viongozi na wadau wengine kuwawezesha Wanawake"
0 Comments