WANAWAKE PEMBA WATAKIWA KUJISHUGHULISHA KATIKA HARAKATI MBALIMBALI ILI KUKUA KIUCHUMI

Wanawake kisiwani Pemba wamewataka wanawake wenzao kujiingiza katika harakati za kujikwamua kiuchumi ili kuepuka kuwa tegemezi kwa familia zao. 

Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi wanawake wa kikundi cha ushirika cha utunzaji mazingira na upandaji miti aina ya mikoko kutoka shehia ya chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wamesema endapo wanawake watajiingiza katika harakati za kimaendeleo kutasaidia kuepuka kuwa tegemezi na kujikwamua kimaisha na kuwa rahisi kuingia katika harakati za uongozi. 
Katibu wa kikundi hicho Fatma Mwadini Shaali amesema ingawa bado hakujawa na kipato kutokana na miti hiyo kuwa midogo lakini wanatarajia mapato mazuri siku za mbeleni. 

Ameeleza kuwa hapo awali katika kikundi chao walikuwa wanajishughulisha na utunzaji mazingira tu lakini baada ya hapo walipata agizo kutoka kwa sheha wao ili wapande na miti aina ya mikoko jambo ambalo limekuwa ni Faraja kwao. 
Kwa upande wake mjumbe wa kikundi hicho Amina Abdala Omar amesema wanatarajia kujiongezea kipato pale tu miti hiyo itakapo kuwa mikubwa kwani watauza mbao na vitu vyengine ambavyo vinatoka katika miti hio. 

Asha kadiru Moh'd amesema miti hiyo yanahifadhi mazingir kwa kuzuzia mmong’onyoko wa ardhi ambayo ni athari kubwa kwa katika jamii. 

Nae afisa kutoka idara ya misitu Wilaya ya Mkoani Gharib Juma Kassim amesema wanaendelea kuwaunga mkono wanawake wa kikundi hicho kwa kuwapatia elimu ya upandaji wa miti na kusaidia kupata vitalu vya misitu,sambamba na kuwapelekea wafadhili ili lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho liweze kufikiwa. 

Kikundi cha utunzaji mazingira na upandaji mikoko kilichopo shehia ya chokocho Wilaya ya Mkaoni kimeanzishwa tarehe 14/2/2025 kikiwa na wananchama 37 wakiwemo wanawake 36 na mwanamme 1.

Post a Comment

0 Comments