TANKI LA KEMIKALI LAPASUKA NA KUSABABISHA BAADHI YA VIFO NA MAJERUHI

Watu kadhaa wamefariki na wengine wamejeruhiwa vibaya baada ya kemikali kuvuja katika kiwanda kilichopo katika Jimbo la Washington, kaskazini-magharibi mwa Marekani.
Taarifa zimesema kemikali hiyo inayojulikana kama "white liquor” ilimwagika baada ya tanki kupasuka, katika kampuni ya Nippon Dynawave Packaging huko Longvie.

Watu wengine tisa wamejeruhiwa katika tukio hilo, wakiwemo wafanyikazi 8 na zimamoto mmoja, Idara ya Zimamoto ya Longview ilisema Jumanne jioni, na kuongeza kuwa bado hali haijatulia.

Mlipuko huo ulitokea kutokana na kupasuka kwa tanki lililokuwa na kemikali , kampuni hiyo ilisema katika taarifa white liquor ni kemikali ambayo hutumika katika ulikaji utengenezaji karatasi.

Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji wa Cowlitz Scott Goldstein amesema eneo la tukio ni shwari,  lakini wananchi wanapaswa kukaa mbali na eneo hilo huku juhudi za kuzima moto zikiendelea ambapo alisema moto huo hauna tishio lolote kwa jamii.

"Eneo la tukio linasalia katika hatua ya uokoaji huku wahudumu wa dharura wakiendelea na kazi," Idara ya Zimamoto ya Longview ilisema katika taarifa.

Kwa sasa hakuna taarifa zozote za kuwatambua watu waliojeruhiwa au waliofariki ambazo zitatolewa kwa kipindi hiki tukisubiri taarifa ya wanafamilia.

Post a Comment

0 Comments