Mwanamke Aliyeandika Historia Zanzibar/ Ukatibu Mkuu Wafungua Fursa Mpya kwa Wanawake.

NA, FATMA SULEIMAN  .
JINA LAKE halisi ni Zena Ahmed Said Mwenye asili ya Kipemba  wazazi wake wote wawili licha ya  maisha kuihamisha familia yake kutoka kisiwa Cha Pemba hadi Mkoa wa Tanga, ni  mke na pia ni mama wa watoto watatu mwanamke mwenye taaluma ya uhandisi.

Zena    alikuwa  katibu mkuu kiongozi na katibu wa baraza la Mapinduzi, alieandika historia kwa mara ya kwanza visiwa vya unguja na Pemba   kushika nafasi hiyo kubwa ya kiutendaji akiwa mwanamke  tangia kuanza kwa awamu ya kwqnza ya uongozi  hadi sasa awamu ya nane.
 HISTORIA YAKE YA KAZI .
" Kabla kuajiriwa serikalini nilianza kazi na kampuni ya Cowl Maswala ya kusimamia ujenzi wa barabara, iliyoanza Tegeta mpka bagamoyo Nikaajiriwa  serikalini na kufanya  kazi wakala wa barabara Tanroads  Tanzania Bara, kwa vile maisha yangu yalikuwa Tanzania bara kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2006 .
Katika kutafutakipato zaidi nilililazimika kuchukua likizo bila malipo na kifanya kazi na World bank na baada ya likizo kumaliza nikarudi tena tanroad hadi mwaka 2016.
FURSA ZA UTEUZI .
Jina la Mhandisi Zena  lilianza kuandika historia ya teuzi   ambapo kupitia Hayati John  Pombe Magufuli  aliteuliwa kuwa  Katibu Tawala mkoa wa Tanga Tanzania wenye Jumla ya wakaazi 2,615,597 . Hadi mwaka 2020, kuteuliwa kuwa  katibu mkuu wizara ya nishati hadi Mwishoni mwa mwezi Disemba  2020.

 Historia  ikaandikwa Zazniabar, kwa mara ya Kwanza Mwanamke kupata nafasi adhimu ya utendaji katika Serikali ya Mapinduzi .
" Tangazo la rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali mwinyi kuniteuwa kuwa katibu wa baraza la mapinduzi   na katibu mkuu kiongozi  lilitoka  na nikaanza kuihudumu kazi hiyo tarehe 2 January  2021 mara baada ya kula kiapo".

JEE KATIBU MKUU KIONGOZI NI NANI NA NI YAPI  HASWA MAJUKUMU YAKE!

Katibu Mkuu Kiongozi ni  mtumishi mkuu wa umma na kiongozi wa makatibu wakuu wote wa wizara.

 Anaongoza na kuratibu utendaji wa utumishi wa umma pamoja na kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Serikali,Kusimamia na kuratibu kazi za makatibu wakuu wa wizara zote,Kumshauri Rais kuhusu masuala ya utumishi wa umma na uendeshaji wa Serikali,Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi na maagizo ya Serikali,Kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na maadili katika utumishi wa umma,Kuratibu shughuli za Serikali zinazohusisha wizara, taasisi na mamlaka mbalimbali,pamoja na Kusimamia masuala ya utawala na utendaji katika Ofisi ya Rais yanayohusu utumishi wa umma.

JEE MHANDISI  ZENA UZOEFU WA UTENDAJI KAZI TANZANIA NA ZANZIBAR  HAUKUWA KIWAZO KWAKWE.

" Muda wangu mwingi nilitenda kazi na majukumu yangu Tanzania bara kuja Zanzibar  kidogo Utamaduni na usimamizi wa majukumu  ulibadilika  kutokana na utamaduni lakini nilisimamia zaidi nidhamu katika utumishi  hali iliyonifanya niome hakuna utifauti wowote Kwa Zanzibar na Tanzania bara katika kusimamia majukumu niliyopewa." 

" Uwajibikaji kwa ninaowasimamia kuna utifauti  kwa kule Tanzania bara na huku Zanzibar  huku kuna muhali sana na sababu kubwa ni ile kuingiliano wa Undugu uliopo takriban taasisi zote"
Nimelisimamia hilo ingawa mpka naondoka bado lipo lakini kidigo limepunguwa   na naendelea kuwasisitiza muhali hauhitajiki ikiwa sheria miongozo na taratibu zipo wazi katika kutekeleza Majukumu.

MHANDISI ATOA FURSA KWA  WANAWAKE WENGINE KUWA VIONGOZI.

 "Dk mwinyi  Rais wa Zqnzibar hahitaji ushawishi katika kuwachaguwa wanawake  na hiyo ilithitika kwa Shirika la UN WOMEN ambao wao waliona Maono  yake ya uwajibikaji na sio jinsia, kwaio kwangu imenisaidia kushauri  tu  katika kuonheza idadi ya wanawake Viongozi yake katika kuamini   walimtambua Dk  kuwa champion kwa Wanawake 
Wengine wanahamasika kupitia kazi zangu tu wanapoziona,  lakini  kwa mwanamke yeyote anataka ushauri maelekezo niseme tu milango kwangu ipo wazi lolote ambalo ninauzoefu nalo bhasi mimi sitosita kusaidia" 
 "Hata kuongea hivi na mimi macho kwa macho bhasi mimi nipo na kunipata ni rahisi  ingawa ratiba zinabana lakini hata kwa njia ya simu lolote ambalo atahitaji kujifunza kupitia mimi mda wowote naweza kufanya hivo Alisema Mhandisi Zena.

NI ZIPI CHANGAMOTO ZA UONGOZI  MWANAMKE HUYU!

" Kwangu hakujawahi kutokea changamoto, kwasababu nafanya kazi na natekeleza majukumu yangu ipaswavyo kwa mujibu wa sheria 
"Ikitokea changamoto kwa yeyote  ambae alikuwa ananiangalia mimi kwa mujibu wa jinsia yangu huyo ni yeye  na sio mimi mimi kikubwa ni heshima hakuna aliewahi kunivunjia heshima katika kusimamia majukumu niliyopewa".

Ninachoamini sijawahi kupata changamoto kwasababu mimi ninakawaida ya kuweka Profesionalisim mbele , namuheshimu kila mtu na nashkuru Alhamdulillah sijawahi kupata chabgamoto kwa sababu ya jinsia yangu"
 Vikwazo vya watu binafsi katika utekelezaji wa majukumi vinatokana na aina ya rasilimali watu  ambao  kwa namna moja ama nyengine huenda labda mtu kapata fursa ya kuchaguliwa kuwa mtu fulani lakini hana sifa au hana vigezo kuweza kufit nafasi aliyonayo"

" Jambo ambalo hupelekea muhali na changamoto katika utendaji, ni vyema  hili liwe linaangaliwa ipasavyo ili kuepusha izo changamoto za muhali katika utendaji kwa baadhi ya watu  wanaotumikia umma "

 Ile tabia ya watu  kujiona ni mabosi wa umma wakati ni watendaji wa umma hupelekea kuongezeka muhali katika utendaji baadhi ya taasisi na mimi katika utekelezaji wa majukumu yangu nilijuwa shida iko wapi wala haikuwa changamoto mana nilijuwa nasolve vipi .

 Alimaliza Mhandisi Zena
Historia hiyo licha ya kuandikwa na Mhandisi zena ambae kwa sasa amepangiwa majukumu mengine ya kiutendaji  kijiti hicho cha nafasi ya ukatibu mkuu kiongozi kimepokelewa na mwanamke mwengine jambo ambalo linaongeza idadi  kutoka mwanamke wa kwanza na kuwa mwanamke aliefungua njia kwa wengine kwenye nafasi hiyo ambae ni Mansura.

Kwa sasa mhandisi Zena ni balozi wa Tanzania nchini Saudia rabia Uteuzi alioteuliwa na Rais  wa Muungano  wa Tanzania  DK Samia Suluhu Hassan

Post a Comment

0 Comments