NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA
Elimu ni moja ya sekta za kipaumbele zilizoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.
Na katika Sera ya Mafunzo ya Elimu (ETP, 2014) ambayo serikali imejitolea kutoa miaka 11 ya elimu msingi bila malipo kwa wote.
Tena hii ni kuanzia elimu ya awali hadi sekondari, yaani kiwango cha kidato cha nne)
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21) unawiana vyema na lengo la 4 la Maendeleo Endelevu la Elimu (SDG 4).
Pamoja na hayo, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika uandikishaji wa elimu ya awali, msingi na sekondari.
Sera ya elimu ya msingi bila malipo ikiwa ni sababu inayochangia.
Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya watoto walio nje ya shule kutokana na matatizo mbalimbali ya ndoa za utotoni na utoro hasa katika maeneo ya vijijini.
Wasichana wana viwango vya juu vya uandikishaji na kubakia katika elimu ya msingi na ya sekondari, lakini wako nyuma ya wavulana katika kiwango cha kutoka ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari.
Hii inaonyesha mwelekeo unaopungua kwa ukuaji wa wanawake kutoka ngazi moja ya juu hadi nyingine.
Ingawa kuacha skuli kunaathiri wanaume na wanawake, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuacha skuli.
Mila za kijamii na kitamaduni kama vile ndoa za utotoni, kazi za nyumbani na ufikiaji mdogo wa habari, kati yawavulana na wasichana ni miongoni mwa sababu zinazosababisha viwango vya kuacha skuli za sekondari ambavyo hutokana zaidi na mimba za utotoni na utoro.
Mambo mengine ni pamoja na umbali mrefu wa kwenda na kurudi skuli, ajira kwa watoto, na unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi ya familia, jamii na shule.
Hivyo, pamoja na jitihada za serikali za kutoa elimu ya msingi bila malipo kwa watoto wote, kiwango cha mpito kutoka elimu ya msingi hadi sekondari, hasa kwa wasichana, bado ni changamoto.
TATIZO
Ndoa za utotoni zimeshamiri nchini Tanzania, asilimia 31 ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza miaka 18 na asilimi 5 huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 15.
Tanzania inashika nafasi ya 11 kwa idadi kamili ya wanawake walioolewa au kuolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na asilimia 4 ya wavulana nchini Tanzania wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Viwango vya ndoa za utotoni vimefikia ni asilimia 59, Shinyanga asilimi 5 Tabora, asilimia 55 Mara ni asilimia 51.
Mkoa wa kaskazi Pemba liliwemo eneo la Micheweni na kisiwa cha Kojani ni moja wapo ya ya maeneo ambavyo wanawake wameonekana kukumbwa na hali hii.
Mwajuma Kombo (sio jana lake) mkaazi wa Micheweni ambaye yeye ni miongoni mwa wathirika aliyekumbwa na ndoa ya umri mdogo, mara baada ya kukatisha masomo.
“Mimi niliolewa nikiwa na miaka 15, na sikuwahi kumaliza elimu ya lazima, maana nilikata njiani na wakati huo wazazi hawakunilazimishi kusoma akijana mume nikpewa,’’anasema.
Anakiri kuwa ndoto zake, zilikatishwa na familia yake, na sasa anaowatoto saba, na wote kama vile wamefuata nyendo za mama yao, kwa kutisha masomo.
Anakiri kuwa, kwa wakati huo wazazi wake hawakuwa na elimu na waliona kama viloe mtoto akienda masomoni, anapoteza mud ana sasa haya ndio matokeo yake.
Mwamvua Sharifu Faki alisema, mila na umaskini ulimfanya yeye kuingia katika ndoa akiwa na miaka13 na hadi sasa akiwa n umri wa miaka 30 licha ya hivyo, lakini hakusita katika kuhakikisha wanawe wanakua katika misingi imara wa kusoma.
Hafasa Haji (sio jina lake) ni mwanafunzi wa skuli ya Chasasa alibebeshwa ujauzito akiwa katika elimu ya msingi, ingawa hadi sasa anaendelea na masomo.
Anasema, uimara wa wazazi wake, baada ya kutokea kwa tukio, lilimpa uimara na sasa anaendelea na masomo.
SERIKAL
Sheria ya Ndoa, Sura ya 29 ya mwaka 1971 kama ilivyorekebishwa mwaka 2019 ni Sheria kuu inayosimamia maswala ya ndoa nchini Tanzania.
Hata hivyo, Sheria hii ni moja kati ya Sheria kongwe nchini Tanzania na imekabiliwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na kuruhusu mazingira fulani ya ubaguzi wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.
Kwa mfano, inawabagua wanaume na wanawake katika uwezo wa kuingia katika ndoa. Pili, Sheria ya Ndoa ina utata katika suala la ugawaji wa mali za ndoa wakati wa talaka, hasa katika ndoa za mitala.
Vile vile Sheria hii inatoa wajibu kwa mume tu kutoa mahitaji kwa ajili ya familia na imeshindwa kutoa tafsiri na adhabu, juu ya masuala ya ukatili hasa wa majumbani.
Sheria ya Mtoto ya Zanzibar nambari 6 ya mwaaka 2011 (Zanzibar Children's Act, 2011): Serikali ilitunga sheria hii maalum ambayo inafafanua mtoto kuwa ni mtu yeyote aliye chini ya miaka 18.
Sheria hii inapiga marufuku aina zote za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, ikiwemo kuozesha Watoto
Ulinzi dhidi ya Unyanyasaji wa Kingono: Sheria za Zanzibar zinatoa adhabu kali kwa mtu yeyote anayehusika kumtia mimba au kufanya mapenzi na mtoto aliye chini ya miaka 18.
Hatua inayosaidia kuzuia ndoa za kulazimishea zinazotokana na mimba za utotoni.
UMASIKINI: Umaskini unachukuliwa kuwa kichocheo kikuu cha ndoa za utotoni nchini Tanzania, Ndoa inachukuliwa kumlinda msichana dhidi ya umaskini na kutoa ahueni kwa familia.
‘’Bei (mahari) ya Bibi Harusi inahusisha mume kutoa pesa, ng'ombe au nguo kwa familia ya bibi-arusi na fursa ndogo za kujipatia kipato, wasichana mara nyingi huona ndoa kama chaguo lao pekee.
MADHARA
Ndoa za utotoni ni aina ya ubaguzi wa kijinsia unaoathiri wasichana wadogo na kuwazuia kuendelea na masomo.
Ukaguzi huo unawafanya waathirika wa maambukizi ya VVU kwa urahisi ikilinganishwa na wapenzi wao ambao hawajaolewa na hakuna uwezekano kwa wasichana hao walioolewa kupanga uzazi.
NINI KIFANYIKE
Kwa kuliona hilo chama cha wandishi wa habari Tanzania TAMWA kimelenga kuisemea jamii kwa kuwapa mafunzo wanadishi wa habari, ili kuonesha sehemu na matukio mbali mbali ya udhalilishaji yanavo athiri jamii na kuto kubadilika.
Program hiyo itakua ni chachu ya wanajamii kuyasemea yale wanayowakwaza na kufika sehemu husika na sharia kuchukuwa mamuzi yake
Asia Hakim ambaye ni afisa amradi wa GBV alieleza kuwa,jamii ya sasahivi inapaswa kukua na kuendana na mabadiliko yaliyopo kwa sasa na kuacha taama ya kuozsha mtoto wako ni kutajirika au kuondosha mzigo.
“Elimu katika jamii tunaendelea kutoa ili kuona jamii imebadilika na kuhamasika katika kujishugulisha kwa kujikwamua kiuchumi.”alieleza.
Bi Siti Faki Ali ambaye mwanaharakati wa kupambana mswala ya udhalilishaji na mshaindizi wa sharia Wilaya ya wete alieleza ni Kua wanachukuwa jitihada za kutosha ili kupambana na janga hilo la mimba za umri mdogo.
Mwisho.
0 Comments