Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amewataka Wanafunzi Wilayani Kisarawe kusoma kwa bidii kwani Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha na kujenga Miundombinu ya elimu bora ikiwemo Mabweni ya Wanafunzi.
Makamu Zainab ametoa wito huo mapema leo Mei 8, 2025 alipokuwa akikagua Jengo la Bweni la Wanafunzi wa Kike katika Shule ya Sekondari Kisarawe iliyopo katika Kata ya Masaki Wilayani humo.
Mradi wa Ujenzi wa Bweni ilo uliogharimu Shilingi Milioni 137 ambapo uwepo wake umewapunguzia Wanafunzi wa Kike umbali mrefu wa Kwenda na kurudi Shuleni,kupunguza tatizo la ndoa na mimba za utotoni ambapo sasa Ufaulu wa Wanafunzi wa kike utaongezeka kutokana na kupata muda mwingi wa kujisomea wakiwa Shuleni.
0 Comments