KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR DKT DIMWA MAZITO AYASEMA KWA WANAWAKE

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa wito kwa wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia katika mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hadi uchaguzi mkuu wa dola Oktoba 2025.
Hayo wakati akizungumza na Kikundi cha Wanawake wa Kikiristo na Maendeleo Zanzibar kanda ya Magharib ‘B’ huko Kiembesamaki Unguja.

Dkt.Dimwa, amesema CCM inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi.
Alisema maendeleo yaliyofikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi yamechangiwa na nguvu kazi ya Wanawake wanaosimamia kikamilifu masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo.

“Natoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wana uwezo wa kuleza mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Dhamira ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki na fursa sawa katika kuimarisha demokrasia.”alisema Dkt.Dimwa.
Aidha, alieleza kuwa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, chama hicho kimeweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kwa njia mbalimbali, ikiwemo mafunzo ya uongozi, uwezeshaji kiuchumi, na kuhamasisha ushiriki wao katika siasa.

Alitoa mfano wa wanawake walioshiriki harakati za kupigania maslahi ya CCM toka wakati wa ASP na TANU ambapo aliwataja waasisi hao ambao ni Bibi Titi Mohamed,Bi.Johari Yussuf Akida na Bi.Mwanaidi Dai.

Katika hotuba yake, Dkt. Dimwa pia alizungumzia umuhimu wa kupinga vitendo vya ubaguzi wa kidini na kikabila, na kuahidi kuwa CCM itaendelea kusimamia haki na usawa kwa wanachama wake wote.

Post a Comment

0 Comments