NAIBU Mrajisi wa mahakama kuu Pemba Faraji Omar Shomari, amekitaka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, ‘ZLSC’ kuongeza kasi zaidi ya kwafuata wananchi maeneo yao, ili kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria.
Alisema, wapo wananchi wamekuwa na umaskini hata wa kutoa nauli ya kuwafuata watendaji wa ‘ZLSC’ hivyo, ili kuwasaidia zaidi, hawana budi kuongeza kasi ya kuwafuta katika vijiji mbali mbali.
Naibu Mrajisi huyo, aliyasema hayo kijiji cha Pondeani shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, wakati akifungua mkutano wa wazi wa kutoa elimu na msaada wa kisheria, ulioandaliwa na ‘ZLSC’ tawi la Pemba.
Alisema, mkutano kama huo ni moja ya hatua kubwa ya kukutana na wananchi moja kwa moja, hivyo ni vyema wakapanga mikakati zaidi ya kuvifikia vijiji vingi.
“Mimi nikipongeze sana Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ kwa hatua hii ya kufunga ofisi na kuamua kuwafuata wananchi, na huku ni kulisaidia kundi kubwa la wananchi kwa wakati mmoja,’’alieleza.
Aidha Naibu huyo Mrajis, aliwataka wananchi kutozifanyia sulhu kesi za jinai, zikiwemo za ukatili na udhalilishaji, na badala yake waziripoti, vituo vya Polisi.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba Safia Saleh Sultan, aliwahimiza wananchi hao, kuendelea kuwatumia wasaidizi wa sheria waliopo katika maeneo yao.
“Kituo kiliamua kuwasomesha wananchi kadhaa katika majimbo yote ya Zanzibar, kwa lengo la kutoa msaada, ushauri na elimu ya sheria kwa wananchi wenzao, tena bila ya malipo,’’alieleza.
Hata hivyo alisema mpango wa kuwafuata wananchi sehemu wanazoishi ni endelevu na ni utamaduni ulioanza muda mrefu, kutokana na wengine kutokuwa na uwezo kukikfikia kituo chao.
Afisa Mipango wa ‘ZSLC’ Pemba Siti Habib Mohamed, alisema wajibu wa wananchi ni kushirikiana na vyombo vya sheria, ili kutokomeza uhalifu.
“Hakuna sheria inayompa uwezo mwananchi kujichukulia sheria mikononi mwake, maana huko ni kuvunja sheria nyengine, kwani kazi ya hukumu kisheria imepewa mahkama,’’alisisitiza.
Sheha wa shehia ya Tibirinzi Mafunda Khamis Ali, aliwataka wananchi wake, kuitumia nafasi hiyo, ili kuelezea matatizo ya kisheria yanayowakabili. Uhuru Gazeti
“Wapo wanaoibiwa mifugo na mazao yao, lakini hata wanaoachwa na kisha kukoseshwa huduma wao na watoto wao, sasa nafasi hii ya kupata ufafanuzi ndio hapa,’’alifafanua. Internews in Tanzania
Wananchi wa Tibirinzi, walisema wamekuwa wakijitahidi kuwafikisha Polisi watuhumiwa wa wizi na wa dawa za kulevya, lakini hawaoni manufaa ya kufanya hivyo. Paralegals Connect
Hamid Said, alisema hawaoni kupungua watumiajia na wasambaazaji dawa za kulevya kijijini kwao, licha ya kuwafikisha watumiwa Polisi mara kadhaa. #ZLSC
Nae Mbarouk Said Juma na Msabah Khamis walisema, juhudi za kuwafikisha watuhumiwa mbele ya vyombo vya sheria, imeanza kupungua kutokana na kuachiwa. Pemba Pressclub
“Labda sasa kuwe na mfumo mpya wa sisi wananchi tusiwe kama mashahidi, na badala yake tuweza kushataki, maana wanaachiwa watuhumiwa kwa vipengele ambavyo ni rahisi kuvieleza mahakamani,’’alieleza. Abdalla J Pangu
Jokha Khamis, alisema hakua anajua kuwa ZLSC inaweza kumpa ushauri na msaada wa kisheria bila ya malipo, na sasa atakuwa karibu kila anapokuwa na kadhia ya kisheria. @Chakechakepa
Zaidi ya wananchi 131 wa shehia ya Tibirinzi kutoka vijiji vya Pondeani, kariakoo, mawasiliano na Pagali walipatiwa elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwenye mkutano huo.
Mwisho
0 Comments