Na mwandishi wetu
Wizara ya elimu na mafunzo amali Zanzibar imekihakishia
chama cha walimu Zanzibar (ZATU) kushirikiana kwa pamoja katika kutatua
changamoto mbali mbali zinazowakabili
katika sekta ya hiyo.
Akifungua kongamano la siku ya walimu duniani katibu
mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis
Abdalla Said kwa niaba ya waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanziba Lela Mohammed Mussa amesema ni haki ya kila mwalimu kuhakikisha anapata
stahiki zake zote ambazo anastahiki .
Amesema wapo baadhi ya walimu wakuu wameshindwa kusimamia
majukumu yao ipasavyo ,hivyo ni vyema kuhakikisha kila mmoja anawajibika katika
majukumu yake .
Aidha amewaomba walimu ambao bado hawajajiunga na chama cha
walimu Zanzibar (ZATU)kuhakikisha wanajiunga na chama hicho ili waweze
kutatuliwa kero zao kwa haraka .
Akitoa salamu za wizara ya elimu Pemba afisa mdhamini wa
wizara ya elimu Pemba Mohd Nassor Salim amesema Zaidi ya walimu 1446
wameajiriwa katika kisiwa cha Pemba kuanzia mwezi Januari mpaka sasa hivo ni jukumu
la walimu kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi Zaidi.
Amesema bado matokeo ya kidato cha nne hayaridhishi kwa
mikoa yote miwili Kaskazini na Kusini Pemba hivo ni jukumu la kila mmoja kwa
nafasi yake kusimamia ili wanafuzi waweze kufanya vizuri.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu Zanzibar wa Chama Cha Mapinduzi Mohd Said Dimwa
ameitaka serikali kuhakikisha inafanya mchakato haraka wa kupatikana tume ya
utumishi kwa ya walimu Zanzibar kabla ya mwaka huu kumaliza.
Ameeleza kuwa lengo la rais wa Zanzibar ni kuona Pemba
inafunguka kama sehemu nyengine kutokana na neema ambayo inapatikana kisiwani
hapa.
Akisoma risala ya walimu kwa mgeni rasmi katibu mkuu wa ZATU
Haji Juma Omar ameiomba Serikali kurejesha nauli za walimu ambao wanaishi mbali
na maeneo ya kazi ili kuweza kufanya kazi kwa ufasi .
Chama cha walimu Zanzibar kimeadhimisha siku ya walimu duniani
katika ukumbi wa chuo kikuu Zanzibar (SUZA)Wete kwa kauli mbiu isemayo ,kuwepo
kwa tume ya utumishi ya walimu Zanzibar kutatatua changamoto zinazowakabili
walimu wa Zanzibar.
0 Comments