Hii ni nguzo ya umeme ama ya mawasiliano mengine, imekatika na kuangukia waya wa umeme, hali ambayo inaweza kusababisha athari kubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo au hata wapita njia. Nguzo hii ipo karibu na barabara kuu kuelekea Kizimbani, mkanyageni (Unguja) hadi kuendelea.

Hapo ni Kianga kwa Humudi (wilaya ya Maghrib A) kabla ya kuvuka daraja. Wito kutoka Zenji Update kwa Shirika la Umeme Zanzibar (Zanzibar Electricity Corporation - ZECO) kufanya jitihada za haraka kuiondoa nguzo hiyo au ili kuikinga jamii kutokana na majanga yanayoweza kusababishwa na hatari hiyo.

Au kama ni makusudi imewekwa hapo kwa sababu za kikufundi au muzijuazo , ni vyema mjukatoa elimu kwa jamii ya maeneo hayo mana wengi wao wanasikitika kwa jambo hilo.

Inapotokea ajali barabarani sio mwendo kasi pekee ndio uliyosababisha ajali hiyo, bali kuangaliwe mazingira mengine huwenda pia yakawa ni sababu ya kutokea ajali hizo.

Kama picha inavyojieleza, mlingoti umebakia mtupu, alama ya barabarani iliyokusudiwa hapo haipo, ikiwa imeharibiwa,kuibiwa au vyenginevyo, lakini ni wajibu kwa mamla husika kuyapitia maeneo hayo mara kwa mara ili kurekebisha kulipokua na kasoro. Milingoti mithili ya hivi ipo mingi barabarani, imebaki mitupu.

Picha inamuonesha mwanamke jinsi alivyochangamka na kazi huko sokoni Jumbi kisiwani Unguja. Nivyema kwa akina mama kuamua kujishirikisha katika harakati za kujipatia kipato kiuchumi kuliko kubaki kua tegemezi katika familia. Umuhimu wake ni kupata fursa za kujimudu katika baadhi ya mambo muhimu katika mahitaji yako.


Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, kilimo ni uti wa mgongo kwako binafsi, anza leo usingoje kesho. Unchokiona ni sehemu maalumu ya kuatika miche mbalimbali kwaajili ya kuiingiza shambani (nasari) Hapo kumeatikwa miche ya mitungule, na eneo kilimo hicho kinafanywa na kijana mdogo ambaye ameanza na msingi mdogo usiyozidi 600,000 na hadi sasa kilimo ndio kinachompatia tija ya kuendesha maisha yake na kuhudumia familia yake.