`

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Tanzania Zanzibar ya mwaka 2022 balozi Muhammad Haji Hamza amesema taarifa za sensa zilizotolewa na watakwimu ipo haja Viongozi kuzielewa na Kuzitumia katika maendeleo ya kijamii Ili kufikia malengo ya sensa hio .

Ameyasema hayo katika kikao Cha utoaji wa takwimu awamu ya tatu ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi mwaka 2022 mkoa WA kusini Pemba.
Kamisaa amesema ni vyema kuwapa uwelewa madiwani pamoja na masheha Ili kuweza kuwashirikisha wananchi katika harakati za kimaendeleo kwa ajili ya maslahi endelevu nchi .
Kwa upande wake mtakwimu mkuu wa serekali Kassim Salum Ali amesema Kila mmoja ana wajibu wa Kuzitumia takwimu zilizotolewa na ofisi ya mtakwimu mkuu wa serekali kwa lengo la kuleta huduma Bora kwa wananchi wote .
Akitoa mada ya matokeo muhimu ya baadhi ya viashiria vya kiuchumi kijamii na mazingira vitokanavyo na sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 Afisa Kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu wa serekali nd Nassir Hamad Salum amesema sensa ya watu na makaazi ilizingatia ngazi zote za kiutawala katika nchi na kuwafikia wananchi wote .
Wakitoa michango baadhi ya madiwani, masheha wamesema kuwa idadi zilizotolewa zinaonesha kuna idadi ndogo wa watoto ukilinganisha na sensa ya awali hivyo kutoa Rai ya kuihamasisha jamii kuzaa Ili kiwango kiweze kuongezeka .