Waziri wa Usafirishaji wa Nchi hiyo, Clemente Beaune amesema atakaa na Wasafirishaji ili kuona njia bora ya kutokomeza uwepo wa kunguni hao huku akiwaahidi abiria hususani wanaotumia vyombo vya usafiri vya umma kwamba usalama wao utalindwa, NBC News na CBS wameripoti. 

Kauli hii ya Serikali inakuja baada ya Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire kuandika barua kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne akimtaka kuchukua hatua za haraka kudhibiti kunguni hao ambao ni hatari kwa afya pale wanampomnyonya damu Mtu lakini zaidi wanalitia aibu Taifa hilo ambalo linajiandaa kukaribisha Wageni mbalimbali mwakani kwenye mashindano na michezo mbalimbali ya Paris Olympics.  

Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionesha kuwepo kwa wadudu hao hasa  katika jiji la Paris kwenye  treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles-de-Gaulle,  Serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.