Ikitokea mke na Mume wameshindwa kupata mtoto Kwa njia ya kawaida na wametafuta Kwa muda mrefu basi muhimu mzingatie na kuyafuata haya::
Hatua ya kwanza:
Mnashauriwa muonane na daktari, mfanye naye mazungumzo na uchunguzi Ili kubaini nini chanzo Cha Ugumba wenu.
Hatua ya pili.,kufanya vipimo vya Afya ya uzazi, Kwa mwanamke vipimo vya kuchunguza nj pamoja na kupima homoni, kupiga utra sound, kuchunguza mlango wa kizazi ,Mirija, mifuko yamayai, kuangalia mji wa mimba( hysterescopy)
Kwa mwanaume vipimo vyake, kwanza kupima mbegu, kama atakuwa na shida itapaswa na yeye kupima kiwango Cha homoni zake, kupiga utra sound, kuangalia mirija na korodani.
Hatua ya tatu: yatapangwa kulingana na matokeo ya vipimo matibabu ya kawaida ikishindikana, upandikizaji wa mbegu, (IUI) Na upandikizaji wa kiinitete (IVF) vinaweza kuhusika Ili kusaidia upatikanaji wa mimba.
Hatua ya mwisho, ni msaada wa kisaikolojia Kwa wanandoa, nimuhimu, huu unaweza kutoka kwa daktari, au watu wa karibu zaidii, nayo muhimu sana.
Je wewe unayesumbuliwa na matatizo ya uzazi, umewahi kwenda na mwenza wako kufanya uchunguzi pamoja?? Au amekutupia mpira wewe tu?
0 Comments