Licha ya Alex Butawantemi (18) mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Tamabu iliyoko Kata ya Tabaruka Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kuendelea kusota rumande akisubiri  hatima ya kupelekwa mahakamani  au laa kwa kosa la kumshambulia mwalimu wake kwa panga akiwa anatekeleza majukumu yake, wakuu wa shule za Sekondari Halmashauri ya Sengerema wamelaani kitendo hicho na  kukiita ni uhaini.

 

Tukio la mwanafunzi huyo Alex Butawantemi (18) kumshambulia mwalimu wake kwa panga lilitokea Sepetemba 25, 2023 shule hapo wakati mwalimu Stanford Mgaya ambaye ni mwalimu wa nidhamu shuleni hapo akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

Mwalimu Zakaria Kahema mkuu wa Shule ya Sekondari Sengerema ni miongoni wa wakuu wa shule  42 za Sekondari waliolaani kitendo hicho na kuwataka wanafunzi wa Sekondari kuachana na makundi ili kuepuka madhara yasiyo ya lazima.

 

"kitendo cha mwanafunzi kumkata panga mwalimu wake kimewasononesha wazazi na walezi sambamba na walimu hivyo wanazitaka  mamlaka husika kuchukuwa hatua stahiki kwa wanafunzi kama hao ambao nidhamu yako ni duni" amesema Kahema.

Mjomba  wa mwanafunzi huyo ambaye ni mlezi  Pamba John akiiangukia Serikali kumsamehe mwanafunzi huyo kutokana na tukio alilofanya, adhabu ya kukaa rumbande  siku Saba hadi sasa ni adhabu tosha ambayo  hawezi kurudia kosa hilo.

Naiomba Serikali kumsamehe mwanangu juu ya tendo alilofanya ambolo kwa kawaida siyo jambo jema alipotokwa , amesema John.

Huku baadhi ya wananchi Wilaya ya Sengerema wakitaka vyombo vya dora kuchukuwa hatua stakihi juu ya mwanafunzi huyo ili liwe fundisho kwa wanafunzi wengine ambao wanaweza kuiga  tabia hizo.

Amos John ni Mkazi wa Kata ya Tabaruka amesema walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Tamabu wasikatishwe tamaa na tukio hili lililotokea shuleni hapo basi waendelee kuchapa kazi na wanafunzi waendelee kusoma ili wafikie malengo yao.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Mwita Waryoba amesema hali ya mwalimu Stanford Mgaya imeimarika wanawashukuru madaktari waliomuhudumia akiwa Hospitari na sasa yuko nyumbani kwake anaendelea vizuri.

chanzo : www.mwananchi.co.tz