Mkuu wa wilaya ya Chakechake Abdalla Rashid Ali ameitaka Jumuiya ya watu wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Zanzibar kuendelea kutoa elimu hasa skulini ili wanafunzi kuipata elimu kwa wakati muwafaka.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa
wilaya Katibu tawala wilaya ya chake chake Suleiman Hamad Suleiman Ameyasema
hayo katika kikao Cha kutoa elimu kwa kwa wazazi , walimu na wanafunzi juu ya
ELIMU ya watoto wanaozaliwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi katika skuli ya
maandalizi madungu chake cheke Pemba.
Amesema kuwa ni vyema jumuiya
kuongeza Juhudi katika kutoa elimu Ili kuondoa changamoto ya uzaliwaji wa
watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Hata hivyo ametoa wito kwa
wazazi na walezi ambao wamepata watoto wenye matatizo hayo hutoa mapenzi na
malezi Bora pasi na kuto kuwanyanyapaa Ili wawe katika makuzi yanayohitajika .
Amesema kuwa na ulemavu kwa
mtoto isiwe sababu ya kupelekea kukosa haki zake za msingi hivyo ni wajibu wa
wazazi kuongeza mapenzi na malezi Bora Ili kujihisi nao ni watu wa kawaida.
Kwa upande wake Afisa mdhamin
wizara ya afya Pemba Khamis Bilali Ali amesema idadi ya watoto wanaozaliwa na
matatizo hayo Zanzibar awali ilikua ni zaidi ya 500 lakini kwa sasa imefikia
475 kutokana watoto 75 kupoteza maisha kwa matatizo mbali mbali.
Amesema kwa unguja Ilikuwa na
watoto 307 na idadi ya watoto hao kwa kisiwa Cha Pemba ilikuwa 120 ambapo
wilaya ya chake ikiwa na watoto 38 mkoani 19 wete 34 na micheweni 19.
Wakitoa elimu kwa wazazi ,walezi
pamoja na wanafunzi Katibu mkuu wa jumuiya hio Hussein Mohd Saleh pamoja na
mjumbe wa jumuiya Ruwaida Ramadhan Saidi wamesema mtu yoyote anaweza kupata
mtoto mwenye matatizo haya kutokana na kukosa mlo kamili hivyo ni vyema kutumia
dawa za folic acid Ili kuzuia uzazi wa mgongo wazi na kichwa kikubwa.
Wakitoa michango baadhi ya
wazazi na pamoja na wanafunzi wamesema ni vyema wanajumuiya kuendelea kutoa
elimu Ili iweze kuwafikia wananchi wote na kuondokana na uzazi wa vichwa
vikubwa na mgongo wazi Zanzibar.
Rmla Makame Juma ambae ni mama wa mtoto mwenye tatizo la
mgongo wazi na kichwa kikubwa amesema watoto wengi ambao huzaliwa na matatizo
haya huchelewa kutembelea na wengine kushindwa kabisa hivyo jambo la muhimu kwa
wazazi ni kuwapa chakula Bora pamoja na mazoezi kwani yanaweza kumjenga na kumrudisha
katika Hali ya kawaida.
Mafunzo hayo yametolewa na Jumuiya ya watu wenye vichwa
vikubwa na mgongo wazi Zanzibar yakiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi na
kuhakikisha ifikapo 2025 kuondoa kabisa watoto vichwa maji na mgongo wazi
Zanzibar.
0 Comments