Kilimo ni eneo ambalo mtu anaweza kufanikiwa haraka ikiwa atatulizanisha akili yake, hivi sasa wengi wa waanchi katika visiwa hivi vya Unguja na Pemba wameshaamka na wameanza kuchangamkia fursa hii. Kilimo cha biashara unaweza kuanza hata kwa mtaji mdogo, yategemea na malengo yako, usiache kufanya kwa kisingizio cha huwezi, badilika, thubutu kufanya utaona mafanikio yake, tija ipo.

Picha zote unazoziona, zimechukuliwa Zanzibar na Camera ya Zenji Update.





Unavyo viona ni makumbi, kamarara, makozi,takataak za baharini ikiwamo, magome ya chaza nk. Bi Maryam wa Mbweni Zanzibar  ameamua kukusanya takataka hizo kugeuza kuwa mapambo yanayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali kupambia, kama vile hotelini, nyumba za kawaida kwa watu wa kawaida na kwengineko.

Anasema ameamua kuja na ubunifu huu, kwa lengo la kuhifadhi mazingira, hasa pale inapoonekana vitu hivyo kuwa takataka, lakini kumbe vinaweza kuwa samani, na pia vikaingiza kipato.