RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendeleza utaratibu wake wa kuwajuulia hali wazee na wananchi kwenye maeneo mbambali kwa kuwaombea dua na kuwatakia kheir na shufaa wagonjwa wapone haraka kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Alhaj Dk. Mwinyi amewatembelea bw. Haji Ramadhan Suweid
Buda, mwandishi wa habari Mwandamizi na Mstaafu kwenye utumishi wa umma na mama
mzazi wa Sheikh Samir Zulfikar wa Mahad el Juneid ya Mkunazini ambao
wanaendelea na matibabu hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Pia, Alhaj Dk. Mwinyi aliwatembelea wazee wa Chama cha
Mapinduzi ambao walitoa mchango mkubwa kwenye chama hicho, akiwemo bw. Kombo
Mzee Kombo nyumbani kwake Miembeni Mkoa wa mjini Magharibi, bw. Bora Afya
Silima Haji nyumbani aliekua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini kichama nyumbani
kwake Mwembelikunda na bi. Hiari Miraji Othman, Balozi wa nyumba 10 namba mbili
huko nyumbani kwake Miembeni jitini.
Mapema, Alhaj Rais Dk. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini
ya Kiislam na wananchi wa Miembeni kwenye ibada ya sala ya Ijumaa kwenye
msikiti wa Ijumaa, Miembeni, Wilaya ya Mjini.
Akizungumza kwenye ibada hiyo Katibu Mtendaji kutoka Ofisi
ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwahimiza waumini wa Kiislam
umuhimu wa tabia njema na kueleza tabia njema ni misingi ya mambo manne ikiwemo
imani.
Sheikh Khalid alieleza, kwenye tabia njema imani hudumu kwa
kutekelezwa amri za Allah (S.W) pamoja na kufuatwa makatazo yake.
Pia, alieleza kukosekana kwa tabia njema imani hupungua na
kuongezeka kwa vitendo vya kuporomoka kwa maadili ikiwemo kupungua kwa heshima
kwenye familia na jamii.
Alisema, siku hizi watoto hawawaheshimu wakubwa zao wakiwemo
wazazi na walezi hata jamii zinazowazunguruka, aliiasa jamii ili kupunguza
wimbi la ukosefu wa maadili na kuepusha athari kubwa za ndoa na takala
zinazojitokeza kwenye jamii ni vyema kutafuta njia za busara ili kukinusuru
kizazi cha sasa kilichogubigwa na wimbi la ukosefu wa heshima na maadili.
Pia, aliiasa jamii kuendelea kuwafundisha mema watoto ili
kukuza jamii yenye heshima, maadili mema na tabia njema.
Kwa upande wake, Khatib wa ibada hiyo ya sala ya Ijumaa aliiasa jamii kwamba uzuri wa waumini
na waislam ni elimu, adabu na kuheshimu viongozi na jamii inayowazunguruka kwa
kujiepusha kutoa maneno yasiyofaa kwa viongozi, wazazi na jamii ili kujenga
jamii iliyonjema.
*IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR*
0 Comments