Na Mwandishi wetu - Pemba

AFISA Mdhamini Wizara ya Biashara  na Maendeleo ya Viwanda, Ali Suleiman Abeid, , amewataka wajasiriamali kisiwani Pemba kutumia mbinu mbalala wanazopatiwa na washirika wa maendeleo, ili kuweza kukuza biashara zao na kupata fursa za masoko  ndani na nje ya nchi.

Akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali Kisiwani Pemba kwenye ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Chake Chake , yalioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania,  amewataka kuchangamkia fursa za masoko zilizo nchini ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa  ujumla.

Kwa upande wake Afisa Biashara kutoka  Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan –Trade) .Feliciana Mbagha amesema  taasisi hiyo imejipanga kufanya utafiti wa masoko utafiti ambao utasaidia kupata takwimu za mwenendo wa biashara nchini.

Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa alama za ubora , Abdalla S Hamad kutoka taasisi ya viwango (ZBS),amewahimiza wajasiriamali kuwa na muamko wa kuhakikisha bidhaa wanazozalisha kukidhi vigezo vya kupata alama ya ubora ili kusaidia upatikanaji wa soko.

Nao wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo , wamesema utaratibu wa utafiti wa masoko utawasaidia kukuza bishara zao.