AJALI SITA (6) ZIMERIPOTIWA MWEZI FEBRUARI, 2025


Jumla ya ajali sita (6) zimeripotiwa mwezi Februari, 2025. Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi ambazo ni mbili (2) sawa na asilimia 33.3 kwa kila Wilaya ikilinganishwa na Wilaya nyengine.
Idadi ya ajali za barabarani zilizotokea kwa mwezi Februari, 2025 zimepungua kwa asilimia 25.0 na kufikia ajali sita (6 mwezi wa Februari kutoka ajali nane mwezi wa Januari, 2025.
Kwa mwezi wa Februari 2025, Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali mbili (2) kwa kila Wilaya na mwezi wa Januari 2025 Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Kati na Chakechake zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali mbili (2) kwa mwezi.
Idadi ya Ajali za barabarani kwa mwaka zimepungua kwa asilimia 68.4 na kufikia ajali sita (6) kwa mwezi wa Februari, 2025 kutoka ajali 19 kwa mwezi wa Februari, 2024.
 Mwezi wa Februari 2025, Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali mbili (2) kwa kila Wilaya na Februari, 2024 wilaya ya Kaskazini ‘A’, Kaskazini ‘B’ na Magharibi ‘B’ zilikuwa na ajali zaidi, ajali tatu (3) kwa kila Wilaya.
Jumla ya waathirika nane  wameripotiwa mwezi Februari, 2025 ambapo waathirika sita (6) ni wanaume na wawili (2) ni wanawake. Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’ zimeripotiwa kuwa na waathirika wengi, waathirika watatu (3) sawa na asilimia 37.5 ikilinganishwa na Wilaya nyengine.
Idadi ya waathirika waliofariki mwezi Februari 2025 ipo sawa na ya mwezi Januari, 2025 (waathirika). 

 Idadi ya waathirika waliofariki kwa mwezi wa Februari, 2025 walioripotiwa  kutoka Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’,  ni waathirika watatu (3) kwa kila Wilaya na mwezi wa Januari, 2025 Wilaya ya Kaskazini B, Kati na Chakechake  waathirika wawili (2) waliripotiwa kwa kila Wilaya.

Waathirika waliofariki  kwa mwezi wa Februari, 2025 wamepungua kwa asilimia 65.2 na kufikia waathirika  nane  kutoka waathirika 23 mwezi wa Februari, 2024. Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘A’ zimeripotiwa kuwa na waathirika wengi waliofariki kwa mwezi Februari, 2025 (waathirika watatu (3) kwa kila Wilaya

Post a Comment

0 Comments